Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi ametembelea familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Kijiji cha Mwitongo, Wilaya ya Butiama, Mkoa wa Mara.
Dk Nchimbi amepata wasaha wa kuzuru kaburi la Mwalimu Nyerere. Ameweka shada la maua, kuwasha mishumaa pamoja na kumwombea mwasisi huyo wa Tanzania.
Mgombea huyo mwenza wa Urais, ametembelea nyumbani hapo leo Jimamosi, Agosti 30, 2025 ikiwa ni siku ya kwanza kuingia mkoani Mara kufanya kampeni za uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika Jumatano ya Oktoba 20, 2025.
Comments