HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI
WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE
Watetezi wa majimbo yao walioanguka 1. Stela Manyanya (Nyasa) 2. Emmanuel Mwakasaka (Tabora Mjini) 3. Charles Kimei (Vunjo) 4. Deo Sanga (Makambako) 5. Antipas (Malinyi) 6. Nagindu Butondo (Kishapu) 7. Joseph Kakunda, (Skonge) 8. Ally Makoa (Kondoa Mjini) 9. Mwarami, 10. Amsabi Mrimi (Serengeti) 11. Benaya Kapinga (Mbinga) 12. Issa Chinguile (Nachingwea) 13. Doroth Kilave (Temeke) 14. Issa Mtemvu (Kibamba) 15. Hassan Mtenga (Mtwara Mjini), 16. Isack Francis Mtinga (Iramba Mashariki) 17. Innocent Bilakwate - Kyerwa 18. Assa Makanika (Kigoma Kaskazini) 19. Vita Kawawa (Namtumbo) 20. Jesca Msambatavangu (Iringa Mjini) 21. Anania Thadayo (Mwanga) 22. Atupele Mwakibete (Busekelo) 23. Joseph Ndaisaba (Ngara) 24. Cosato Chumi (Mafinga) 25. Joseph Kizito Mhagama (Madaba) 26. Maimuna Mtanda (Newala V) 27. Stanslaus Nyongo (Maswa Mashariki) 28. Marco John Sallu (Handeni Mjini) 29. Dkt. Daniel Pallangyo (Arumeru Mashariki) 31. Prof. Patrick Ndakidemi (Moshi Vijijini) 32. Exhaud K...
NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE
Alhamdulillah ala kulli hal Nimepokea uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa moyo wa shukrani. Quran Tukufu inatufundisha kuwa Allah ndie mpangaji na ni bora kwetu. ALHAMDULILLAH Ndugu zangu wanaTanga Mjini, nitumie fursa hii kuwashukuru kwa kuniamini kuwa Mbunge wenu kwa kipindi cha miaka 5 (2020 - 2025) Nafurahi kuona kuwa utumishi wangu kwenu umewagusa wengi na umeacha alama kubwa za kimaendeleo katika Jimbo letu. Asanteni kwa ushirikiano mzuri mlionipatia ktk kipindi chote cha Utumishi wangu. Kwa dhati ya moyo wangu, ninawashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum wa CCM Wilaya ya Tanga kwa kunipa kura nyingi ktk mchakato wa kura za maoni za kutafuta mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo letu Tanga Mjini kwa kipindi cha 2025 - 2030. Mlinikopesha imani kubwa sana Nitaienzi na kuithamini imani hii daima. UAMUZI wa vikao vya Chama ni lazima UHESHIMIWE. Nampongeza Ndugu Kassim Amar Mbaraka (Makubel) kwa kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM Tanga Mjini. Ninawaomba wanakimji wen...
SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia leo August 06,2025 akiwa anaendelea kupatiwa matibabu Hospitalini baada ya kuugua ghafla. Kwa mujibu wa taarifa ya Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson aliyoitoa imesema: “Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika mstaafu wa Bunge, Job Ndugai kilichotokea leo jijini Dodoma. “Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Kongwa, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.” Dk Tulia amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na kamati ya mazishi pamoja na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Ndugai amekuwa Spika wa Bunge tangu November 17, 2015 hadi Januari 06, 2022 alipojiuzulu na kuendelea kuwa Mbunge wa Kongwa nafasi ambayo ameendelea kuitetea kwa kuchukua fomu tena mwaka huu ambapo ameshinda kwenye kura za maoni.
WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI
1. Ummy Mwalimu - Tanga. 2. Stanslaus Mabula - Nyamagana 3. Shaban Mrutu - Tabora Mjini 4. Malecela - Dodoma. 5. Luqman Merhab - Mufindi Kastazini 6. Kirumbe Ng' enda - Kigoma. 7. Alexander Mnyeti - Misungwi 8. Prof Edwinius Lyalya - Magu. 9. Robert Maboto - Bunda. 10. Fredrick Lowassa - Monduli. 11. Munde Tambwe - Sikonge
WALIOSHINDA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA
MTOKO MPYA WA YANGA HUU HAPA
KILUNBE NG'ENDA ATEULIWA KUWA NAIBU KATIBU MKUU JUMUIYA YA WAZAZI CCM
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC), Wilson Elias Mulumbe (katikati) aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Shoka Khamis Juma (kushoto) katika tukio lililofanyika Agosti 14, 2025 Njedengwa jijini Dodoma. Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuchukua fomu, Mgombea pendekezwa wa Urais wa chama hicho, Mulumbe amesema kuwa chama chake kikishinda atahakikisha anafuta madeni yote wanayodaiwa wanafunzi na Bodi ya Mikopo, itakuwa elimu bure, afya bure na wateja wataunganishiwa umeme bure. Vyama vingine vilivyochukua fumu jana Agosti 13, 2025 ni; Chama cha Democratic Party (DP), Abdul Juma Mluya (Urais) aliyeambatana na Mgombea Mwenza, Masoud Abrahman Khatib na Cha...
CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-
"Miaka 12 iliyopita nilipata fursa ya kujifunza diplomasia na ustahimilivu kupitia aliyekuwa Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa [SUKI] Dr. AshaRose Migiro. Alinitaka muda wote kutenda kwa kuandaa maandiko na kuyasaili kisha ndipo nitende. Shule ile ilinikaa na kunifanya muda wote nikikutana naye hata baada ya kuhama ofisi moja na nyingine nimkumbuke kama mwalimu imara. Miaka imeenda na siku zikasonga mbele." "Leo ameaminiwa kushika nafasi ya juu ya utendaji ya CCM. Nafasi ambayo nami nilishaitumikia kabla ya mtangulizi wake. Hakika nimefurahi kuona Mwalimu akikabidhiwa darasa kufundisha. Kazi muhimu ni wanafunzi kubeba utayari. Karibu tena nyumban SG mpya." "Sisi tupo tayari kutumwa. Picha hii ni kumbukumbu ya mimi na SG mpya katika mkutano Mkuu uliopita." #KaziNaUtuTunasongaMbele #NaendeleaKujifunza
Comments