NI SHANGWE TUPU MAPOKEZI YA DK.NCHIMBI WILAYANI ITILIMA SIMIYU

Wakazi wa Kata ya Langabilili,wilaya ya Itilima mkoani Simiyu leo Jumanne Septemba 2,2025 wamejitokeza kwa wingi kumpokea na kumkaribisha kwa shangwe Mgombea Mwenza wa Urais wa   Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiendelea na ziara mkoani Simiyu.

 Dkt.Nchimbi amepokewa kwa shangwe na Wananchi wa Langabilili,ndani ya jimbo la Itilima, huku wakionesha shauku kubwa ya kutaka kumuona na kumsikiliza katika mkutano wake wa Kampeni.

Dk.Nchimbi ambaye alitokea mkoani Mara na sasa ameingia mkoa wa Simiyu kuendelea na mikutano ya kampeni katika Mkoa huo,baada ya kutoka Busega,Bariadi Vijijini na sasa ameingia jimbo la Itilima  kufanya mkutano mkubwa wa Kampeni
 
Akiwahutubia wananchi katika stendi ya Mabasi ya Langabilili, Itilima mkoani Simiyu, katika muendelezo wa mikutano yake ya Kampeni,Balozi Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Itilima,Njalu Daudi Silanga sambamba na Wagombea Ubunge wengine pamoja na Madiwani wa Mkoa huo.

Katika mkutano wa kampeni Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi pamoja na mambo mengine amekuwa akiinadi Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM Rais Dk.Samia Suluhu,Mgombea mwenza wa Urais,wabunge na madiwani wa Chama hicho.


Dkt. Nchimbi anaendelea na kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa huku akinadi Sera na Ilani ya chama hicho 2025-2030 kwa Wananchi, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania  kuwaongoza katika awamu nyingine ya miaka mitano, katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.








Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI

RAIS SAMIA AMUONDOLEA POLEPOLE HADHI YA UBALOZI