Shamrashmra katika mkutano wa KAMPENI za Mgombea URAIS kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan mjini Tunduma Leo Septemba 3,2025.
Akiwa katika mkutano huo, Dkt. Samia atajinadi kwa kuelezea mafanikio makubwa ya maendeleo aliyoufanyia mkoa huo mchanga au kitinda mimba lakini vilevile kutoa ahadi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Akiwa katika mkutano huo, Dkt. Samia atajinadi kwa kuelezea mafanikio makubwa ya maendeleo aliyoufanyia mkoa huo mchanga au kitinda mimba lakini vilevile kutoa ahadi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Pamoja na kuelezea kwa ndani Ilani ya uchaguzi ya chama hicho, Dkt. Samia ambaye mgombea wake mwenza ni Dkt. John Nchimbi, atatumia fursa hiyo kuwanadi wagombea ubunge na madiwani wa chama hicho.
Baadhi ya miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na itakayotekelezwa katika mkoa huo ni kama ifutavyo;1.Ujenzi wa barabara kuu ya Tanzam Kwa njia 4 kuanzia Igawa(Mbeya) Hadi Tunduma(Songwe) km 218
2.Ujenzi wa barabara ya Ruanda/Iyula (Tanzam Jnct)-Nyimbili-Itumba-Isongole(Malawi Border) km 79.6
3.Ujenzi wa barabara ya Mahenje-Vwawa km 32
4.Ujenzi wa barabara ya Mlowo-Kamsamba km 130 &Utambalila-Chitete Bypass
5.Makongolosi-Chang'ombe-Mbalizi
6.Isongole-Isoko km 52
7.Ujenzi wa Tunduma Dry Port(Mpemba)
8.Miradi wa Uchimbaji Madini Adimu(Ngualla Rare Earth Project)
9.Mradi Wa Uchimbaji wa Dhahabu Wilaya ya Songwe
10.Ujenzi wa Maegesho ya Kisasa ya Malori Chimbuya.
-
11.Ujenzi wa Vwawa-Mpemba-Nkangamo Bypass
12.Ujenzi wa Chuo Cha Mifugo Mbozi
13.Iboya Onestop Inspection Centre
14.Ujenzi wa Makao Makuu ya TRA & TanRoads
15.Ujenzi wa Mradi mkubwa wa Umeme wa Grid ya Taifa kuunganisha na Zambia Mbeya-Tunduma-Sumbawanga kv 400
16.Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe
17.Tawi la Chuo Cha Ufundi DIT Myunga Campus
18.Ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Ileje.
19.Mradi wa Maji Itumba-Isongole
20.Ujenzi wa Chuo Cha VETA cha mkoa
Miradi aliyoikamilisha Rais Samia ni;
-Ujenzi wa Hospital ya Mji Tunduma
-Ujenzi wa barabara ya Mpemba/Tunduma-Isongole km 50
-Ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya ya Momba,Songwe na Mbozi DC
-Ujenzi wa Makao Makuu ya Mkoa Bwawa
Miradi ambayo Iko mbioni 'pipeline' ni;
-Upembuzi yakinifu wa Vwawa na Tunduma Bypass
-Upembuzi yakinifu wa mradi mkubwa wa Maji kutoka Mto Momba Hadi Tunduma,Bwawa na Mlowo (over 320bln)
-Songwe Airport
-Songwe River Hydropower Project.
Miradi hiyo mikubwa itakapokamilika itainua uchumi wa Mkoa wa Songwe na kuleta ustawi kwa wananchi wake na Taifa Kwa ujimla.
Kesho Septemba 4-5, 2025 ataendelea kupeperusha bendera katika Mkoa wa Mbeya katika Mji wa Mbarizi na Mbeya Mjini katika Uwanja wa Ndege wa zamani eneo la Mwanjelwa. Siku yake ya pili atafanya mikutano Rungwe Mashariki,wilayani Mbarari katika Mji ya Ubaruku na Igawa baada ya hapo ataelekea mkoani Njombe.
Comments