BASHE AMSHUKURU MUNGU, ATOA SHUKRANI KWA RAIS



Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini na aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, ametoa kauli yake rasmi muda mfupi baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutangaza Baraza jipya la Mawaziri kwa mwaka 2025–2030, ambapo jina lake halimo katika orodha ya walioteuliwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bashe ameanza kwa kumshukuru Mungu na kuonesha shukrani kubwa kwa Rais Samia kwa imani aliyooneshwa kwake katika kipindi cha awamu ya kwanza ya uongozi wake, akimpa nafasi kwanza kama Naibu Waziri, kisha Waziri wa Kilimo.


“Ni heshima niliyothamini kwa moyo wangu wote, na ninaendelea kuwa mwenye shukrani kwa nafasi hiyo ya kuwatumikia Watanzania,” ameandika.


Akimpongeza Waziri mpya wa Kilimo, Daniel Chongolo, Bashe amesema anamfahamu kama “mzalendo na mkulima,” na anaamini atamsaidia Rais kutimiza matarajio ya Watanzania.


Pia amempongeza Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, akisema hana mashaka naye na anamfahamu kama “mzazi na mtu atakayekuwa msaada mkubwa kwa waziri wake.”


Katika salamu zake, Bashe pia ameushukuru uongozi mzima wa Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano waliompa kwa kipindi cha miaka sita alichohudumu, akiwatakia heri katika kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya taifa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

WALIOCHUKUA FOMU CCM ZA KUWANIA USPIKA HAWA HAPA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MATOKEO YA DARASA LA 7 YATANGAZWA

MJUE VIZURI KOCHA MPYA WA YANGA PEDRO

JESHI LA POLISI LATEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA, LAONDOA KIZUIZI CHA KUTOTOKA NJE BAADA YA SAA 12 JIONI