MSIGWA AVIPASHA UKWELI VYOMBO VYA HABARI VYA NJE

"Tunapoendelea kusubiri tume hii ikamilishe kazi yake kumejitokeza wimbi kubwa la vyombo vya habari hususani vyombo vya nje kuchapisha na kutangaza taarifa ambazo ni za upande mmoja na wakati mwingine kufanya upotoshaji wa taarifa wenye mrengo wa kuchochea chuki kwa Watanzania dhidi ya serikali, kuwagombanisha Watanzania wenyewe kwa wenyewe kutokana na tofauti zao-kisiasa kidini na kikanda.


 Serikali ama viongozi wa serikali akiwemo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inasikitishwa na imeumizwa sana na matukio yale na madhara yake. Kuendelea kushabikia matukio yale hakuna manufaa kwa taifa letu zaidi ya kuongeza maumivu katika vidonda vya Watanzania naomba kueleza yafuatayo. Naomba kutoa wito kwa vyombo vya habari vya nje kuzingatia maadili na misingi ya vyombo vya habari kwa kuchapisha habari zinazozingatia usawa haki na uwajibikaji".

"Sio haki na sio sawa kwa chombo cha habari kuchapisha taarifa za upande mmoja na kisha kutoa sababu kuwa maafisa wa serikali walipotafutwa hawakupatikana kama ambavyo chombo cha habari cha CNN kilivyochapisha habari zake zilizojaa tuhuma pasipo kutoa nafasi ya serikali kujibu", Msigwa.

Hayo ameyasema Gerson Msigwa Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Michezo Sanaa na Utamaduni  leo Novemba 23, 2025 akizungumza na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

WALIOCHUKUA FOMU CCM ZA KUWANIA USPIKA HAWA HAPA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

MJUE VIZURI KOCHA MPYA WA YANGA PEDRO