MKUU wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka, amewataka viongozi, Taasisi za dini kutumia nyumba za ibada kujenga jamii yenye maadili na hofu ya Mungu.
Aidha, amewasihi Wazazi waendelee kushirikiana na Viongozi dini na Taasisi za kidini kujenga vijana wenye malezi Bora kwa Taifa. Hayo aliyasema kwenye hafla maalum ya uchangiaji wa ujenzi wa Msikiti, katika Kijiji cha Mvumi kilichopo wilayani humo, amesema Taasisi za kidini zimekuwa na mchango makubwa katika kuendeleza na kukuza vijana kimaadili. Amesema Viongozi waendelee kujenga vijana wenye hofu ya Mungu na wenye maadiili mazuri, wenye kumjua Mungu. Shaka amesema Watanzania kwa ujumla kuendelea kuliombea taifa na kudumisha amani, utulivu na mshikamano.
Aliwataka pia Wazazi kuliombea taifa liendelee kudumu katika amani, utulivu na mshikamano na kuwa tathmini iliyofanyika hivi karibuni imeonesha kuwa Tanzania ndiyo nchi ya kwanza Afrika ya Mashariki kuwa na utulivu na amani, jambo ambalo linapaswa kudumishwa. "Wazazi, Viongozi mna mchango mkubwa katika taifa hili, katika kujenga maendeleo na ni mfano wa kuigwa pia wazazi tushikamane na viongoz wa dini. " Niwaombe wazazi wenzangu kujenga malezi bora kwaajil ya kujenga taifa hili, ili tuweze wa na vijana wenye hofu ya Mungu" Amesema Shaka. Akizungumzia ujenzi wa Msikiti huo Mwenyekiti wa Taasisi ya Almasjdi liqadiria Tanzania Sheikh Mahmoud Waziri, katika Taasisi yake ina vijana zaidi ya 400 ambao wapo kwenye makundi tofauti tofauti . Amesema licha ya kufundisha dini, wanaendeleza ni pamoja na kuwa na walimu, maafisa utendaji na wauguzi. Waziri amesema amefurahishwa na ujio wa mgemi rasmi pamoja na Viongozi mbalimbali waliojitokeza kushiriki katika zoezi la uchangiaji ambalo kwa asilimia kubwa limefanikiwa. " Naishukuru Serikali ya Rais Samia Hassan Suluhu, imetoletea Kiongozi mtu wa watu, amekuja kwenye jambo letu la uchangiaji, tumefanikiwa kwa asilimia kubwa, ameonyesha upendo wa dhati kwenye, tunaendelea kumuombea yeye na Taifa letu kwa jumla" Amesema. Mwisho

Comments