Dhamira ya Tanzania kuendelea kudumisha amani inachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi, kuvutia uwekezaji wa ndani na kimataifa, kuchangia ustawi wa maendeleo ya Bara la Afrika na dunia kwa ujumla.
Jitihada hizi zimekuwa zikihujumiwa na baadhi ya watu wasiolitakia mema Taifa letu akiwemo Bw. Godbless Lema kwa kujaribu kufanya ushawishi wa kuvuruga jitiahada hizi kwa kushirikiana na wanaharakati waliopo nje ya Tanzania wanaotumia mitandao ya kijamii kujaribu jenga ushawishi hasi kwa wananchi.
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inaeleza kuwa Tanzania kama mpatanishi wa kuaminika na kupitia ushiriki wake katika michakato ya amani katika Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki ina jukumu la kuendelea kudumisha amani kwa nguvu zake zote.
Hata viongozi wetu wa dini wameonesha kwa uwazi dhamira ya kuwaleta pamoja watanzania na kuleta maridhiano, umoja, kudumisha amani kwa sababu huo ndio Msingi wa jukumu lao walilokabidhiwa na Mwenyezi Mungu kuwahudumia binadamu kimwili na kiroho. Tunawashukuru kwa kuendelea kwa moyo huu, Ishara wazi kwamba tutavuka hata katika kipindi hiki tunachopitia baada ya Oktoba 29, 2025.
Pamoja na viongozi wetu hawa wa kiroho wa dini zote kuendelea kutekeleza jukumu lao la kutukumbusha umuhimu wa amani hapa nchini bado wamezuka watu wachache akiwemo ndg Gobless Lema ambaye bila haya jana kupitia ukurasa wake wa mitandao ya Kijamii alionekana kukejeli akauli iliyotolewa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Singida Dkt Cyprian Hilinti aliyetoa wito kwa Watanzania kulinda amani iliyopo nchini, akisisitiza kuwa bila amani hakuna shughuli yoyote ya uzalishaji, kiuchumi, kidini wala kijamii inayoweza kuendelea.
Kwa muktadha huo, kama Kiongozi wa Dini kosa lake ni nini hapo? Au ndio tuseme ndugu Lema umejipa jukumu la kuwa Kiongozi wa viongozi wa Dini, tunakutambua kama Mwanasiasa uliyepoteza mwelekeo, umejikita katika kutafuta kuungwa mkono na viongozi wa dini kwa manufaa yako na wale wanaokusaidia kufanya siasa za maji taka. Tambua kwamba Askofu Hilinti ni mtu anayeheshimika katika jamii na Msomi mwenye mangamuzi na dhima ya kuhubiri amani na sio uanaharakati kama unafanya Lema.
Askofu Hilinti alisisitza kuwa “Kwenye amani, tunafunga ndoa, tunafanya kazi zetu, tunaabudu kwa uhuru, tumekusanyika hapa kwa sababu ya uwepo wa amani, alihoji kama sio amani je shughuli za kiibada zingweza kufanyika, shughuli za kilimo mashambani nazo zisingeweza kufanyika”, alisema Askofu Dkt Hilinti
Sasa ndugu Lema wewe unataka kusiwe na amani ili shughuli za wananchi zisiendelee au tukueleweje? Nadhani viongozi wetu bado wana wajibu wa kuendelea kutupa miongozo ya kuufuata ili kuepuka mtego tuliowekewa na adui zetu wanaowatumia watanzania wenzetu kama Lema ambaye ana uraia wa Canada.
“Ukosefu wa amani haumuthiri kiongozi, chama cha siasa au kundi Fulani la watu bali ni taifa zima litashindwa kuendelea kwa sababu ya kukosekana kwa amani, hivyo ni jukumu la kila mtanzania kuilinda na kuidumisha kwa nguvu zake zote,” alisema Askofu Dkt Hilinti

Comments