WENYEJI, Yanga SC wameanza vyema hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco jioni ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee katika mchezo huo wa kwanza wa Kund B, mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Mpumelelo Dube dakika ya 58 akimalizia pasi ndefu ya kiungo mzawa, Mudathir Yahya Abbas.
Hii inakuwa mara ya kwanza kihistoria Yanga kushinda mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakiposhiriki kwa mara ya kwanza mwaka 1998.
Mechi nyingine ya Kundi B Ligi ya Mabingwa itafuatia Saa 1:00 usiku baina ya mabingwa wa kihistoria, Al Ahly na JS Kabylie ya Algeria Uwanja wa Al Salam Jijini Cairo nchini Misri.
Yanga SC sasa itasafiri kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa pili wa Kundi hilo dhidi ya wenyeji, JS Kabylie Novemba 28 Uwanja wa Hocine Aït Ahmed mjini Tizi Ouzou siku ambayo FA Rabat watakuwa wenyeji wa Al Ahly Uwanja wa Prince Moulay Abdellah Stadium Jijini Rabat.
@mgadafiprince.73
@yangasc

Comments