CHATANDA ANGURUMA IDODI, AWAFIKISHIA SALAMU ZA RAIS SAMIA NA KUMPIGIA DEBE MTATIFIKOLO JIMBO LA ISMANI.


Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), anaendelea hamasa yakuzitafuta kura za CCM kwa kufanya Vikao vya Ndani mkoani Iringa leo Mei 26, 2026 katika kata za Mahuninga na Idodi.

Katika vikao hivyo vilivyohusisha makundi mbalimbali wakiwemo wanawake wajasiriamali, vijana, maafisa usafirishaji, mabaraza ya kata, matawi, na mabalozi. Chatanda amewafikishia wana-Ismani salamu za upendo na shukrani za pekee kutoka kwa Jemadari wetu, Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Rais ameshukuru kwa kura zote za kishindo na uaminifu mkubwa walioonyesha kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025, uliompa ridhaa ya kuendelea kuiongoza na kuijenga Tanzania. Hatua iliyomwezesha kuunda serikali madhubuti inayoendelea kutekeleza ilani ya CCM.

Pia, ametoa wito kwa wana-Ismani kumchagua Ndg. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda kama mbadala thabiti na chaguo sahihi la kuwaletea maendeleo ya kweli kupitia CCM. Amesisitiza kuwa Kaganda ndiye mbadala thabiti na chaguo sahihi lenye maono, atakayeshirikiana bega kwa bega na Serikali ya Awamu ya Sita kuwaletea maendeleo ya kweli na ya kasi wananchi wa Ismani kupitia tiketi ya CCM.





 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI