Mgeni Rasmi:
Mhe Dr Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tarehe:
22.8.2026
Utaungulizi:
Serikali za awamu zote 6 zilisimamia tafiti na maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme kwenye Mto Rufiji, eneo la Stiegler's Gorge.
Mradi ulianza tokea kwenye maono ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere miaka ya 1970, na kuendelea kuratibiwa kwenye uongozi wa Hayati Rais Ali Hassan Mwinyi, na Hayati Benjamin William Mkapa.
Uongozi wa Mhe Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete uliendelea na tafiti, tathmini za mazingira na maandalizi ya mradi kwa uwezekano wa kushirikisha sekta binafsi.
Ujenzi ulianza rasmi kwa kuwekwa Jiwe la Msingi tarehe 26.7.2019 na Hayati Rais Dkt John Pombe Magufuli
Ukamilishaji na uzinduzi rasmi wa uzalishaji wa umeme (JNHHP) wa MW 2,115 uliofanywa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan jana tarehe 22.8.2026
Mradi wa JNHPP umekamilika kwa gharama ya takribani Tsh trilioni 7.5 zilizofadhiliwa asilimia 100 na Serikali yetu.
Picha za hapa:
1. Picha ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya kutambua mchango wake mkubwa kwenye ukamilishaji wa mradi wa JNPP wa kuzalisha umeme wa MW 2,115
Mhe Rais alikuwa pamoja na Mawaziri walioshiriki kwa nyakati tofauti kwenye upangaji na utekelezaji wa mradi huu, hao ni: Prof Sospeter Muhongo, Dkt Medard Kalimani, Ndugu January Makamba, Dkt Doto Biteko na Ndugu Deogratius Ndejembi
Marais wa awamu zote 6 wamepewa Tuzo za ushiriki wao mkubwa kwenye mradi huu mkubwa wa kuzalisha umeme kwenye Mto Rufiji (JNHHP) wa MW 2,115
2. Prof Sospeter Muhongo, Dr Medard Kalimani na Ndg January Makamba wakiwa kwenye sherehe ya uzinduzi wa JNHPP
3. Prof Muhongo na Injinia Masanja (Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Nishati) wakiwa wamesimama na Wafanyakazi wa TANESCO kwenye hafla uzinduzi wa JNHPP
Picha zimeambatanishwa hapa
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P.O.Box 6
Musoma
Date: Sun, 23 August 2026
Comments