MSUNGU AREJESHA FOMU ZA KUOMBA KUGOMBEA UMAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA

 Kada wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Daud Msungu (kushoto), akirejesha fomu za kuomba kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti wa umoja huo, kwa Sophia Duma ambaye ni Mkuu wa Idara ya Organaizesheni Makao Makuu ya UVCCM, Dar es Salaam leo. Msungu alikuwa mjumbe wa Baraza la umoja huo kupitia Mkoa wa Lindi.
                                                  Msungu akionesha fomu alizozirejesha

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kurejesha fomu hizo, Msungu, alisema endapo akifanikiwa kugombea na kushinda wadhifa huo, atamshauri mwenyekiti, kuweka mikakati ya kuwashawishi vijana kushiriki katika ujenzi wa uchumi na maendeleo ya Taifa, kwa vile vijana ndiyo nguvu ya Taifa.

Pia amesema kuwa, atahakikisha wanarudisha umoja na mshikamano kwa vijana kwa ajili ya ustawi wa Chama Cha Mapinduzi.

"Hiyo itasaidia vijana kusukuma mbele, gurudumu la maendeleo ya Taifa letu, kuendana na kasi ya  kiuchumi na maendeleo hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kiuchumi yanayoendelea duniani" alisema Msungu.

Atashirikiana na viongozi wengine wa umoja huo, kuandaa mipango ya mafunzo kwa vijana kuielewa vizuri itikadi ya chama, hasa kwa kufufua vyuo mbalimbali vya itikadi ikiwemo Kambi ya Ihemi, mkoani Iringa.. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA