Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka.
Kamishna wa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul Kinemela (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akikanusha taarifa zilizotolewa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), zilizodai Serikali inampango wa kupunguza mafao ya Pensheni ya Wanachama wa Mifuko ya LAPF na PSPF. Kulia ni Kamishna wa Kazi Msaidizi, David Kanali na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Juma Muhimbi.
Kamishna wa Kazi Msaidizi, David Kanali, Juma Muhimbi, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari.
Meneja Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika akimkaribisha Kamishna wa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul Kinemela, kuzungumza na wanahabari.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya SSRA wakiwa kwenye mkutano huo.
Wakurugenzi wa SSRA wakiptia taarifa hiyo ya kukanusha taarifa iliyotolewa na CWT.Imeandaliwa na www.habari za jamii.com)
Wakurugenzi wa Idara mbalimbali wa SSRA wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Matekelezo na Uandikishaji, Lightness Mauki, Mkurugenzi wa Tehama, Carina Wangwe, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani, Peter Mbelwa na Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Rasilimali Watu, Mohamed Nyasama
Mkurugenzi wa Sheria wa SSRA, Ngabo Ibrahim (katikati), akiandika taarifa hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka na Meneja Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imekanusha tamko liliotolewa na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisiza Elimu (THTU) na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) la kudai kwamba kuna mpango wa kupunguza Mafao ya Pensheni ya wanachama mifuko ya LAPF na PSPF.
Akizungumza Dar es Salaam leo Kamishna wa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul Kinemela alisema taarifa hizo sio za kweli ambazo kwa namna nyingine zinalenga kupotosha umma.
''Tunaomba wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii na umma kwa ujumla kuwa kinachoendelea ni majadiliano na wadau wa sekta ya hifadhi ya jamii yenye lengo la kuboresha mafao ya wastaafu'' alisema Kinemela.
Alisema kuwa Chama cha Walimu Tanzania ( CWT) na THTU wakiwa ni wadau sekta ya hifadhi ya jamii wanayo haki ya kikatiba ya kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali yakiwamo ya sekta ya hifadhi ya jamii.
Alisema Serikali inachukua fursa hiyo kuwatoa hofu wastaafu na wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
''Tunaomba wadau wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa watulivu na kujiepusha na maneno yoyote ya upotoshwaji na mwisho kuwachanganya wanachama na hivyo kupunguza ufanisi wa kazi na utendaji,'' alisema Kinemela.
Comments