KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA KIWANDA CHA KONYAGI. MKURUGENZI AITAKA SERIKALI KUACHA KUPANGA KODI BILA MPANGILIO


 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Luhaga Mpina akipata maelezo kutoka kwa Meneja Ufundi wa kiwanda hicho, Khadija Madawili kuhusu utengezaji wa konyagi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi Tanzania (TDL), David Mgwassa (kulia) akizungumza katika mkutano na wabunge wa  Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara,  walipotembelea kiwanda hicho, Dar es Salaam juzi, ambapo alilamikia kitendo cha serikali cha kupandisha kodi bila mpangilio hivyo kusababisha uendeshaji wa viwanda kuwa mgumu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi Tanzania (TDL), David Mgwassa (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Deo Ndunguru (kulia) pamoja na Mbunge wa Viti Malumu, Naomi Mwakyoma (Chadema)
 Meneja wa Ufundi wa Kiwanda cha Konyagi Tanzania (TDL),Khadija Madawili  akiwaeleza wabunge wa  Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara,kuhusu utendaji wa kiwanda hicho walipotembelea kiwanda hicho, Dar es Salaam
 Wabunge wa kamati hiyo na maofisa wa wizara ya viwanda na biashara wakitembelea kiwanda hicho
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi Tanzania (TDL), David Mgwassa (kulia) akizungumza katika mkutano na wabunge wa  Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara,  walipotembelea kiwanda hicho, Dar es Salaam juzi, ambapo alilamikia kitendo cha serikali cha kupandisha kodi bila mpangilio hivyo kusababisha uendeshaji wa viwanda kuwa mgumu.

Na Richard Mwaikenda
UONGOZI Kiwanda cha Konyagi Tanzania (TDL), umelalamikia kitendo cha Serikali kupandisha kodi bila mpangilio, hali inayosababisha uendeshaji wa viwanda kuwa mgumu.

Malalamiko hayo yalitolewa na Mkurugenzi wa kiwanda hicho, David Mgwassa mbele ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara walipotembelea kiwanda cha TDL, jijini Dar es Salaam jana.

"Kodi, kodi, kodi, hakuna mtu anaogopa kulipa kodi, lakini kodi iwe na mpangilio. Kwa mfano mwaka huu
Waziri wa Fedha alitangaza bungeni na kwenye vyombo vya habari, ongezeko la kodi asilimia 10, Muswada wa Fedha (Finance bill) ukawa asilimia 20, halafu muswada huo unasainiwa na Rais, Julai 3, 2014 na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali Julai 11, 2014 na Mamlaka ya Mapato inaanza kuwadai wenye viwanda kuanzia Julai Mosi. Je hiyo ni halali?" Alisema Mgwassa na kuhoji.


Alisema pia kuwa wenye viwanda wanaelemewa na kodi kubwa zilizo nje ya bunge, wanazotozwa na wakala na mamlaka mbalimbali kama vile, Mamlaka  ya Udhibiti Sumatra, Ewura, WMA, REA, TBS, Zimamoto na Uokoaji Fire and rescue , TFDA. Vilevile na kodi zinazotengezwa na sheria ndogo za halamashauri na manispaa za miji.

Mgwassa aliiomba serikali kusaidia kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazokikabili kiwanda hicho, hasa wanaposafirisha bidhaa katika nchi jirani za Kenya, Msumbiji na Zambia ambapo magari yaliyobeba bidhaa zao hukwamishwa mpakani hadi kufikia wiki mbili kwa visingizio vya vibali.

Alisema kwa upande wa Kenya ambako hivi sasa kinywaji chao cha konyagi kina soko kubwa, mtu akifa kwa kunywa pombe ya huko inayofanana na gongo, hutangaza kwenye vyombo vyao vya habari kuwa amekufa kwa kunywa konyagi, lakini serikali ya Tanzania kupitia ubalozi wetu Kenya inakaa kimya.

Akijibu Hoja na malalamiko hayo, Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge, Luhaga Mpina, alisema kuwa malalamiko hayo watayajadili kwenye vikao vya kamati za bunge vinavyoendelea kwa lengo la kuyapatia ufumbuzi.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Maria Bilia, aliomba uongozi wa kiwanda hicho, umpatie nyaraka mbalimbali zinazoonesha unyanyasaji wanaposafirisha bidhaa nchi jirani ili zifanyiwe kazi na kuzipatia ufumbuzi.

Mgwasaa alisema kiwanda hicho ambacho kiko chini ya ubia wa Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Sabmiller cha Afrika Kusini, kinachangia uchumi wa Tanzania kwa kulipa ushuru na kodi zaidi ya sh. bil. 500 kwa mwaka.

Wajumbe wa kamati hiyo walioongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Luhaga Mpina walitembelea kiwanda hicho na kujionea jinsi vinywaji mbalimbali vinavyotengenezwa kwa kutumia mitambo ya kisasa.





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA

NOTI MPYA KUANZA KUSAMBAZWA MWEZI UJAO