SERIKALI YA MKOA WA IRINGA YAANZA MCHAKATO WA KUPASUA BARABARA ITAKAYOUNGANISHA MKOA WA MOROGORO NA IRINGA KUPITIA KILOLO

Mbunge  wa Kilolo Venance  Mwamoto akiwa  kijiji  cha Mhanga kata ya Kimara wilaya ya Kilolo mkoani Iringa akionyesha wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro ,wilaya  ya Kilolo ipo mbioni kuunganishwa kwa barabara  na wilaya ya Kilombero
 Meneja  wa wakala  wa baraba (TANROAD) mkoa  wa  Iringa mhandisi Daniel Kindole(kulia) akimsikiliza mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto (kushoto )  wakati wa  ziara  ya  kukagua eneo  ambalo Tanroad watachonga barabara  kati ya  kijiji  cha Mhanga  wilaya ya  Kilolo na Mgeta wilaya ya  Kilombero mkoa wa Morogoro 
 .................................................................................................................................................

Na MatukiodaimaBlog

SERIKALI ya  mkoa  wa Iringa  ipo mboni kupasua barabara mpya  itakayounganisha wilaya ya Kilolo na  Kilombero mkoani Morogoro kama  njia  ya  kuwakwamua  kiuchimi wananchi  wa kata za pembezoni  na wilaya ya Kilolo.

Meneja  wa wakala  wa baraba (TANROAD) mkoa  wa  Iringa mhandisi Daniel Kindole akizungumza leo  na  viongozi  wa seriikali ya kata ya Kimara baada ya  kufika kutazama eneo  ambalo barabara   hiyo itapita ,alisema  kuwa ziara  yake  katika wilaya  hiyo ni utekelezaji  wa maagizo  ya  kikao  cha bodi ya barabara  mkoa kufuatia maombi ya  mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto katika  kikao hicho  kutaka wanachi  wa Kilolo waunganishwe na  wale wa Kilombero.

Mhandisi Kindole  alisema baada  ya  kufika  eneo hilo ameona  upo  uwezekano mkubwa  wa barabara   hiyo  kutengenezwa ili  kuunganisha wilaya ya  Kilolo mkoa  wa Iringa  na wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Hivyo  alisema kwa kuwa barabara hiyo kikao  cha bodi ya barabara na  kile  cha kamati ya  ushauri ya  mkoa  waliagiza kufika kutazama eneo  hilo kwa upande wake ametekeleza na atarejesha majibu  ili vikao hivyo  vya mkoa  kuweza  kuingiza barabara hiyo katika  orodha  za barabara za mkoa  .

Huku mwenyekiti  wa serikali ya kijiji cha Mhanga  Bw Emelis Kiongozi pamoja na  kumpongeza mbunge wao  kwa  kufikisha maombi ya  wananchi katika  vikao  vya  mkoa bado alisema  kuwa ujenzi  wa barabara  hiyo utasaidia  kufungua milango ya uchumi katika  wilaya ya Kilolo  kwa kusafirisha mazao yao hadi Morogoro .

Aliasema  iwapo barabara  hiyo ya Mhanga hadi Mgeta  wilaya ya Kilombero itafunguliwa itakuwa na faida   kubwa kwa wilaya ya Kilolo kwani  alisema ni  mwendo  wa masaa 3 kutoka Iringa mjini hadi Morogoro kama barabara   hiyo  itafunguliwa ila kwa sasa wanatumia  zaidi ya masaa 10  kutoka kijiji  cha Mhanga Kilolo kwenda Morogoro kupita barabara  ya Kilolo- Iringa .

Mbunge  wa Kilolo Bw Mwamoto  alisema  kuwa kufunguka kwa barabara  hiyo kutakuza uchumi  wa  Kilolo na mkoa mzima  wa Iringa kwani miongoni mwa  wawekezaji  wakubwa katika  wilaya ya Kilolo ni pamoja na kampuni ya New Foresti inayojihusisha na  kilimo  cha miti hivyo  barabara   hiyo itawawezesha  kusafirisha mazao  hayo ya miti kwenda Mgeta wilaya ya  Kilombero ili  kutumia  usafiri wa gari moshi (Treni)

"Hawa  wawekezaji  itakuwa  rahisi  kwao  kusafirisha  mbao na magogo kwenda kijiji  cha Mgeta ambako ni Kilomita 20 pekee ili  kutumia usafiri wa Treni kusafirisha  kwenda Dar es Salaam na mikoa mingine badala ya kuzunguka hadi Iringa mjini  zaidi ya Kilometa 60 "alisema Mwamoto  

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO SABA AMBAYO WANAUME WENGI HAWAYAPENDI:

NI HESHIMA KUBWA SANA KUIFUNDISHA YANGA - KOCHA MPYA WA YANGA

UOKOAJI KARIAKOO NI USHUHUDA WA MOYO WA UTANZANIA: NCHIMBI

”RAIS SAMIA AUMIZWA MAUAJI YA KIBIKI”

KOCHA SEAD RAMOVIC AMRITHI GAMONDI YANGA.

TAMISEMI PUUZENI DOSARI NDOGONDOGO ZA WAGOMBEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA - DK. NCHIMBI

RAIS SAMIA ATOA SALAMU ZA POLE KWA KIFO CHA DKT. NDUGULILE

CCM YASAMBAZA VIONGOZI NA MAKADA WAANDAMIZI NCHI NZIMA