MAMBO SABA AMBAYO WANAUME WENGI HAWAYAPENDI:



Katika Mambo haya Hakuna yametofautiana kutokana na aina ya maisha mnayoishi na mumeo lakini wanaume wengi wapo hivi.


1__.MWANAMUME HAPENDI KUFOKEWA:


 Hata Kama amekosea; jaribu kumuonyesha kosa lake pasipo kumfokea au kumvunjia heshima.


2__ MWANAMUME HAPENDI KUULIZWA MASWALI MENGI KWA WAKATI MMOJA:


 Ukimuuliza swali halafu yeye anakua kimya au anaduwaa; ujue hana jibu au anajisikia vibaya kuhusu jibu ambalo anatakiwa kutoa. Mpe muda ajipange kutoa jibu usimlazimishe siyo mtumwa wako.


3__ MWANAMUME ANAHITAJI MUDA WA KUKAA KIMYA; USIMLAZIMISHE KUONGEA:


 Zaidi sana anapopita kwenye hali ngumu au changamoto fulani; wanaume wengi hupenda kukaa kimya huku akiwaza nini cha kufanya. 


Tofauti na wanawake, ambao wakati wa changamoto ndipo wanataka kuongea zaidi.

 Wanaume wengi hawapendi kuongea kama hawana suluhisho la shida iliyopo mbele yao hivyo Kama wewe ni mtu sahihi kwake jifunze kumsoma mumeo ili ujue nyakati zake ngumu ili usimame kwenye zamu yako.


4__ MWANAMUME HAPENDI MKE MWENYE KIHERE-HERE:


Yani hata kama bado hajakwambia, kaa ukijua kwamba wanaume hawapendi kuwa na mke ambaye hapitwi na jambo.

 Mwanamke anayetaka kuchangia kila kitu au kuongea-ongea sanaaaa! Mmmhhh! Unamchosha mwanamumeo.


5__ MWANAMUME HAPENDI MKE WAKE AWE NA MARAFIKI WEEENGIII; KIBAYA ZAIDI SANA ETI NI MARAFIKI WA KIUME: Wanaume wengi wana WIVU; (NA HIYO NI ASILI YAO) 


Hivyo mwanamume hapendi kuona mke wake yuko bize “ku-entertain” wanaume wengine (HATA KAMA HAKUNA MAHUSIANO MABAYA).

 Mara huyu ni rafiki yangu tulisoma nae, niliwahi fanya nae training, ni mwalimu wa kwaya, oohh huyu tulifanya nae kazi, bla, bla , bla zako zitakuvunjia mji tumia akili ipasavyo.


6__ MWANAMUME HAPENDI KUNYANYASIKA:


 Wanaume wengi ni rahisi kusumbuliwa na hali au hisia ya kujiona duni (Inferiority Complex). 


Zaidi sana kama MKE ndiye mwenye kipato kikubwa, au elimu kubwa, umri mkubwa, au anatoka familia yenye nguvu zaidi kuliko ya mume. ( Lakini ni kwa hasiyejiheshimu)

Hapo inabidi mwanamke awe makini sana maana kitu kidogo tu kinaweza sababisha mwanaume adhanie kwamba tayari anadharaulika. Mwanamke anahitaji HEKIMA ya juu kuishi na mume mwenye shida ya kujidharau.(Faida ya MKE MWENYE HEKIMA inatenda kazi Sana mahali hapa)


7__ MWANAMUME, HAPENDI KUPOTEZA MAMLAKA AU SAUTI YAKE KWA MKE WAKE:


 Mwanamume akiona dalili za kupoteza mamlaka yake na kukosa sauti kwa mkewe, basi hujaribiwa kutafuta mahali pengine pa kuonyesha hiyo mamlaka.( MCHEPUKO)


Ni rahisi KUMPENDA Mke mwenye UTII ;Vilevile, ni rahisi KUMTII Mume mwenye UPENDO


#Kila MWANAMKE aliye na HEKIMA HUJENGA nyumba yake; Bali aliye MPUMBAVU HUIBOMOA NYUMBA YAKE kwa mikono yake MWENYEWE


JIFUNZE MENGI KWAKUJIUNGA NA GROUP WASP.


0769228130


MWANAMKE NA NDOA BORA


Uchumba na ndoa Bora.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

NI HESHIMA KUBWA SANA KUIFUNDISHA YANGA - KOCHA MPYA WA YANGA

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

”RAIS SAMIA AUMIZWA MAUAJI YA KIBIKI”

KOCHA SEAD RAMOVIC AMRITHI GAMONDI YANGA.

UOKOAJI KARIAKOO NI USHUHUDA WA MOYO WA UTANZANIA: NCHIMBI

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE