YANGA YAIFUMUA APR 2-1 RWANDA


TIMU ya Yanga leo imthibisha kuwa wao ni wa kimataifa baada ya kuitandika APR mabao 2-1 katika mchezo wa Klabu bingwa Afrika uliochezwa kwenye dimba la Amahoro.

Kipindi cha kwanza APR ilifika langoni mwa Yanga mara nyingi lakini walionekana wazi kuzidiwa mbinu na walinzi wa ngome ya Yanga iliyoongozwa na Vicent Bossou na Kelvin Yondan. 

Dakika ya 20, Juma Abdul aliwainua mashabiki wa Yanga kwa bao safi kufuatia shuti kali la mpira wa adhabu ndogo uliotinga moja kwa moja nyavuni huku kipa wa APR, Kwizera Oliver akichupa bila mafanikio.



Kipindi cha pili APR waliliandama lango la Yanga lakini umakini wa mabeki wa wanajangwani hao pamoja na kipa Ally Mustapha uliwanyima bao wanajeshi hao.


APR walioonyesha kuchanganyikiwa kadiri dakika zinavyokwenda, almanusura wapate bao katika dakika ya 55 baada ya beki mahiri Rwatubyaye Abdul kuachia shuti kali ambalo lilimgonga Pato Ngonyani kabla mpira huo haujaokolewa na mabeki wa Yanga. Wachezaji wa APR walimzonga mwamuzi wakidai Pato aliunawa mpira huo.

Heka heka langoni mwa Yanga ziliendelea huku Yanga wakiongeza umakini na kucheza kwa tahadhari wakiumudu vema mfumo wao wa 3-5-2. 

Mashambulizi ya kushtukiza yalionekana kuiletea faida Yanga kwani katika dakika ya 74, Thaban Kamusoko aliipatia Yanga bao la pili akimalizia pasi nzuri ya Donald Ngoma.


Katika dakika za nyongeza, Patrick Sibomana aliiandikia APR bao la kufutia machozi hivyo mchezo huo kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kwa ushindi huo Yanga wamejitengenezea mazingira mazuri ya kuitoa APR kwani katika mchezo wa marudiano jijini Dar watahitaji japo sare tu kuiondosha timu hiyo mashindanoni.


MPIRA UMEKWISHAAA

-GOOOOOO Dakika za majeruhi, Patrick Sibomana anaifungia APR bao moja. Ulikuwa mpira wa krosi, Barthez akaruka na kuudaka lakini wakati anashuka chini akauachia. Sibomana katikati ya mabeki wa Yanga Bossou, Yondani na Juma Abdul, akafunga akiwa ametulia kabisa

-Mugenzi anapoteza nafasi ya wazi kabisa baada ya krosi safi kutoka Magharibi ya uwanja
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89, nusura Msuva afunge bao la tatu baada ya kipa na mabeki wa APR kujichanganya
SUB Dk 87 Yanga inamtoa Niyonzima na kumuingiza Mbuyu Twite
KADI Dk 85, Juma Abdul analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Bizimana
Dk 83 Emiry anapiga mpira wa adhabu unavuka ukuta wa Yanga lakini Barthez anadaka vizuri kabisa 
Dk 81, APR wanapata kona ya saba katika kipindi cha pili pekee, anaichonga Iranzi, lakini inakuwa haina manufaa kwa mara nyingi. APR sasa wanaonekana kutoka mchezoni zaidi wanafanya ubabe tu

DK 80, Free kick, Juma Abdul anapiga vizuri kabisa, hata hivyo anashindwa kulenga lango
KADI Dk 78 Emiry Bayisenge analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ngoma 

Dk 77 APR wanapata kona nyingine baada ya Yanga kuokoa, lakini inaonekana haina matunda
GOOOOOO Dk 74, Kamusoko anaifungia Yanga bao la pili baada ya Juma Abdul kumpa pasi Ngoma aliyempasia mfungaji kwa ulaini kabisa
Dk 71 sasa bado inaonekana mpira zaidi unakuwa wa kubutua, unachezwa zaidi katikati ya uwanja na Ngoma leo anaonekana kutokuwa na mchango mkubwa na amepooza sana
Dk 67 sasa, kinachoonekana Yanga wamepoozesha mchezo lakini APR wanashambulia zaidi na sasa wamepata kona tano katika kipindi cha pili pekee

Dk 66, kona safi ya APR inachongwa na Bernabe anapoteza nafasi nyingi ya wazi wakati Barthez akiwa amelala chini baada ya kugongwa
Dk 64, Yanga wanapata kona ya kwanza katika kipindi cha pili, hata hivyo inakuwa ni dhaifu na isiyo na matunda
Dk 60, Yanga wanafanya shambulizi kali la kipindi cha pili, lakini APR wanaokoa na mpira unagonga mikono ya Msuva

KADI Dk 57 Iranzi analambwa kadi ya njano kwa kumsukuma Yondani kwa makusudi
Dk 55 APR wanapata kona ya pili, shuti kali linapigwa lakini mpira unaokolewa na pato Ngoyani anayepiga kichwa shuti hilo linalomwangusha, yuko chini anatibiwa

Dk 51 APR wanatumia muda mwingi kucheza mpira katika eneo lao. Bado inaonekana hata Yanga pia hakuna mashambulizi makubwa wanayofanya na kusababisha mpira kuonekana umepoa sana
Dk 48, Iranzi kabisa lakini Yondani anaokoa na kuwa kona lakini haina matunda

Dk 47 krosi nzuri Rutanga anaiwahi na kuugonga mpira lakini Barthez anauwahi na kudaka vizuri
SUB Dk 46 Yanga inamtoa Tambwe ambaye mwanzo ilielezwa ni majeruhi na nafasi yake inachukuliwa na Simon Msuva 

MAPUMZIKO
Dk 45, Juma Abdul anafanya uzembe mkubwa, Mwinyi anaokoa na kuwa kona. APR wanapiga lakini Barthez anaruka safi kabisa na kudaka vizuuuriii

Dk 42 Bizimana ambaye ni mjomba wa Niyonzima anapoteza nafasi nzuri kabisa ya kufunga baada ya kuruka na kushindwa kupiga kichwa akiwa pekee analiangalia lango la Yanga
Dk 37, Juma Abdul anaruka kupiga kichwa krosi safi ya Mwinyi, hata hivyo anashindwa kuufikia mpira, anafanya madhambi

Dk 34, shuti kali la kwanza kumfikia kipa linapigwa na Iranzi, lakini Barthez anaonyesha umahiri kwa kudaka vizuri kabisa
Dk 32, Juma Abdul analala chini baada ya kuumia, Pato Ngonyani ndiye aliyemkanyaga kwa bahati mbaya wakati wakiwania mpira
Dk 29, Iranzi anaonekana kulalamika, kwamba hakumuangusha Niyonzima ambaye alikuwa akiwachambua. Niyonzima anaonekana kupania kuonyesha mambo mengi katika mechi hii ambayo amerejea nyumbani akiwa na Yanga
Dk 22, Bernabe maarufu kama Balotelli anaruka juu na kupiga kichwa safi kabisa, lakini kinakuwa hakina nguvu na Barthez anadaka kwa ulaini kabisa
GOOOOOOOOO Dk 20 Juma Abdul Jaffar anaiandikia Yanga bao la kwanza kwa mpira safi wa faulo

Dk 18, Juma Abdul anakunja krosi safi kabisa, lakini hata hivyo inakuwa juu kidogo, Tambwe anashindwa kuiwahi
Dk 12 hadi 14, bado inaonekana ni mechi ya kuviziana, kidogo beki wa kushoto wa Yanga, Mwinyi Haji anaonekana kutotulia vizuri na ndani ya dakika mbili amepoteza mipira mitatu

Dk 11, kona ya kwanza ya mchezo, APR ndiyo wanaopata lakini inaokolewa vizuri hapa na Yondani
Dk ya 10 sasa, bado hakuna timu iliyoonyesha kuwa na mpango madhubuti katika ushambulizi. Huenda ni hofu ya mwanzo ya mchezo huku APR wakionekana kupoteza sana mipira
Dk 9, Bernabe wa APR naye katika nafasi nzuri pembeni ya uwanja anapiga shuti la hoovyoo kabisa
Dk 4, Kaseke anajaribu kupiga shuti lakini linakuwa dhaifu kabisa
Dk 1, APR ndiyo wanaanza pambano kwa kasi, lakini Yanga wanaonekana kuupoza mpira



KIKOSI CHA APR
1. Kwizera Oliver  
2. Rusheshangoga 
3. Michael  Rutanga 
4. Eric Rwatubyaye 
5. Emiry Bayisenge
6. Yannick Mukunzi
7. Fisto Kinzingabo
8. Jihadi Bizimana (Mpwa wa Haruna) 
9. Mubumbyi Bernabe 
10. Iranzi Jean Claude (C) 
11. Patrick Sibomana. 

#Subs 
1.Ndoli Jean Claude 
2.Rwigema Yves 
3.Usengimana Faustin 
4.Nshutinamagara Ismael 
5.Benedata Jamvier 
6.Mugenzi Biemveni 

7.Ntamuhanga Tumaini

KIKOSI CHA YANGA:
1. Ally mustapha
2. Juma abdul
3. Mwinyi haji
4. Calvin yondani
5. Vincent bossou (C)
6. Pato ngonyani
7. Deus kaseke
8. Thaban kamusoko
9. Hamis tambwe
10. Donald ngoma
11. Haruna niyonzima

Formation 3:5:2

Subs
1. Deo munis
2. Oscar joshua
3. Mbuyu twitte
4. Issouf boubakr
5. Salum telela
6. Matheo anthony
7. Simon msuva

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA