UJENZI WA BARABARA ZA JUU UBUNGO DAR KUANZA MARA MOJA

From Town:


From Kimara:


Sam Nujoma - Nelson Mandela (upper floor):


FYI:
Images grabbed from the simulation as presented
Kazi kwenu...
Better but still unde

Soma hii:
‘Flyover’ Ubungo

Akizungumzia barabara hiyo ya juu ya Ubungo, Mkuu Idara ya Usanifu na Viwango wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Ebenezer Mollel alisema katika eneo la Ubungo kutakuwa na barabara za ngazi tatu ambazo zitakuwa katika mifumo isiyowezesha msongamano wa magari.

Mollel alisema barabara za mabasi yaendayo haraka (BRT) itaendelea kufanya kazi kama kawaida ikiongozwa na taa, huku magari yanayotoka barabara ya Sam Nujoma na Mandela, mfano Buguruni - Mwenge au Mwenge - Buguruni yatakuwa yakipita juu.

“Katika barabara ya kwanza magari kutoka mjini (Barabara ya Morogoro) kwenda Buguruni (Mandela) na Kimara (Morogoro) kwenda Mwenge (Sam Nujoma) yataongozwa na taa. Magari yanayotoka Buguruni kwenda Mwenge na Kimara kwenda Buguruni nayo yatafuata mfumo wa taa,” alisema Mollel.

“Katika barabara ya pili magari yanayotoka mjini (Barabara ya Morogoro) kwenda Mwenge na Kimara kwenda Buguruni nayo yatatakiwa kuongozwa na taa na hii ‘Flyover Interchange’ haitakuwa na msongamano kwani kila gari litakuwa na njia yake na hakutakuwa na msongamano wowote.”
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakisaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
PICHA NAMBA 2

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakisaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakibadilisha hati za mikataba mara baada ya kusaini ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akitoa maelezo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange) utakaotekelezwa na kampuni M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC).
Baadhi ya wawakilishi wa Mkandarasi wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) wakifuatilia hafla ya utiaji saini ya ujenzi wa Ubungo interchange Jijin Dar es salaam.

Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), leo umetiliana saini na kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) mkataba wa  ujenzi wa barabara za Juu ‘Interchange’ katika makutano ya barabara ya Sam Najoma na Mandela Ubungo jijini Dar es salaam.
Mkataba huo unamtaka Mkandarasi kampuni ya CCECC kutoka China kuanza ujenzi huo mara moja na ujenzi huo unatarajiwa kutumia takriban miezi 30 hadi kukamilika kwake.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale amesema zaidi ya shilingi Bilioni 177.4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo utakaowekewa jiwe la msingi mwezi machi mwaka huu.
“Hakikisheni mnaanza ujenzi mara moja kwani Serikali imeshakamilisha taratibu zote na tayari kiasi cha shilingi bilioni 2.1 kimelipwa kwa ajili ya fidia kwa wananchi walioguswa na mradi huo”. Amesema  Eng. Mfugale.
Ujenzi wa Ubungo interchange unajengwa kwa fedha ya mkopo kutoka Benki ya Dunia ambapo Serikali kwa upande wake imeshalipa fidia ya zaidi ya shilingi bilioni 2.1
“Zaidi ya magari 65,000 yanapita kila siku katika katika makutano ya barabara za morogoro,Mandela na sam nujoma eneo la Ubungo hali inayosababisha msongamano katika barabara ya Morogoro ambayo ndio lango kuu la kuingia jijini Dar es salaam  hivyo ufanisi wa mradi huo utahuisha hali ya usafirishaji katika jiji la Dar es salaam na kuchochea ukuaji wa uchumi” amesisitiza Eng. Mfugale.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CCECC Bw, Jiang Yigao amemhakikishia Eng. Mfugale kuwa wataanza maandalizi ya ujenzi huo mara moja na watafanya kazi hiyo kwa wakati.Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA