MRADI WA MABASI YA MWENDO KASI KUHARAKISHWA MBAGARA, GONGO LA MBOTO, TEGETA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Mabasi  ya Mwendokasi Dar es Salaam (DART), Ronald Lwakatare akielezea kuhusu mafanikio ya mradi huo katika mkutano wa kimataifa wa maendeleo ya uchumi wa kijani, Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Mabasi  ya Mwendokasi Dar es Salaam (DART), Ronald Lwakatare akielezea kuhusu mafanikio ya mradi huo katika mkutano wa kimataifa wa maendeleo ya uchumi wa kijani, Dar es Salaam
 Wajumbe wa mkutano huo wakisikiliza kwa makini

 Lwakatare akizungmza na mwandishi wa habari mwanadamizi wa gazeti la Jambo Leo, Suleiman Msuya katika Hoteli ya Kilimanjaro, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi Dar es Salaam (DART) Ronald Lwakatare

Suleiman Msuya
MKURUGENZI wa Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi Dar es Salaam (DART) Ronald Lwakatare amesema wanatarajia kuongeza mabasi ya mwendokasi 165 katika njia 10 za kuingia mitaani (Fider roads), katika maeneo yanayopakana na barabara ya Morogoro.

Aidha, amesema mradi wa DART unatarajiwa kuendelea katika njia ya Mbagala, Gongo la Mboto na Tegeta ili kuweza kukamilisha njia zote husika na kupunguza foleni jijini Dar es Salaam katika kipindi cha miaka mitano hadi 10.

Lwakatare aliyasema hayo jana wakati akizungumza na JAMBOLEO jijini Dar es Salaam ambapo alishiriki katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu kukuza mazingira ya kijani katika miji unaondelea hapa nchini.

Alisema mkakati wa Serikali kwa kushirikiana na mwekezaji ni kuona huduma ya usafiri wa mwendokasi inamfikia kila mwananchi anayeishi Dar es Salaam.


Mkurugenzi huyo alisema ongezeko hilo la njia zinazoingia mitaani litahusu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mwenge, Sinza, Masaki, Sinza, Kawe, Barabara ya Mandela na nyingine nyingi.

Alisema kwa sasa magari ni machache hivyo mpango uliopo ni kuongeza magari katika njia hizo ili kukamilisha mpango mzima wa awamu ya kwanza.

“Kwa sasa mabasi ni machache hivyo tunatarajia kuongeza mengine 165 ambayo yataingia njia za mitaani kama Sinza, Mwenge na zingine ambazo zinakutana na barabara ya DART,” alisema.

Alisema mradi huo wa awamu ya kwanza umekuwa na mafanikio ya hali ya juu kwani wananchi wamekuwa wakitumia nafasi kubwa kupumzika tofauti na zamani ambapo walikuwa wanadamka usiku.

Akizungumza awamu ya pili ya mradi wa DART ambao unaelekea Mbagala, alisema unatarajiwa kuanza wakati wowote mwaka huu kutokana na 
ukweli kuwa fedha zipo ila kinachosubiriwa ni zabuni kutangazwa na mkandarasi kupatikana.

Lwakatare alisema kuna uwezekano mradi wa awamu ya pili ukaenda sambamba na mradi wa awamu ya tatu ambao utahusu njia ya Gongo la Mboto na wa nne wa njia ya Tegeta.

Alisema matarajio yao ni kuona miaka 10 ijayo jiji la Dar es Salaam litakuwa limeondokana na msongamano wa foleni ambayo inakwamisha shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Aidha, alitoa wito kwa wananchi kutunza miundombinu ya DART ili iweze kudumu na kutumiwa na vizazi vijavyo kwani fedha zinatumika kulipa deni hilo ni kodi za wananchi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

MAMBO SABA AMBAYO WANAUME WENGI HAWAYAPENDI:

NI HESHIMA KUBWA SANA KUIFUNDISHA YANGA - KOCHA MPYA WA YANGA

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

”RAIS SAMIA AUMIZWA MAUAJI YA KIBIKI”

KOCHA SEAD RAMOVIC AMRITHI GAMONDI YANGA.

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE

UOKOAJI KARIAKOO NI USHUHUDA WA MOYO WA UTANZANIA: NCHIMBI