Wananchi wakiangalia ajali ya Coaster iliyobeba wananfunzi wa iliyoporomoka korongoni eneo la Mlima Rhotia wilayani Karatu Arusha wakati wakielekea kwenye ziara ya kimasomo.ambapo zaidi 30 walikufa kwenye ajali hiyo wakiwemo pia walimu Wanafunzi hao walikuwa wanatoka Shule Lucky Vincent Nursery & Primary School ipo Arusha ni medium schools
WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO
WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amepiga marufuku wasiosomea masuala ya Kilimo kuuza pembejeo. Amesema kuwa masharti ya muuza pembejeo lazima awe amesomea Kilimo kwa ngazi ya cheti, diploma na Digrii. Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na wadau wa mbegu katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma. "Haiwezekani wanaowashauri na kuwauzia mbegu wakulima wasiwe na utalaamu wa sekta hiyo, mbona wanaogawa dawa na kutibu wagonjwa wamesomea ufamasia, uuguzi na udaktari, kwa nini isiwe kwenye Kilimo? Amehoji Waziri Bashe. Amewapa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja wauzaji kwenda kusomea Kilimo ili waruhusiwe kisheria kuuza Pembejeo na kwamba baada ya hapo sheria itafuata mkondo wake kwa kukagua maduka yote ya pembejeo na kuwakamata watakaobainika.
Comments