Rais John Magufuli akikutana na wakuu wa mikoa katika kikao kilichohudhuriwa pia na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, baadhi ya mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju Ikulu jijini Dar es salaam
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK
OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza
Wakuu wa Mikoa kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa viwanda
katika maeneo yao ili kuwawezesha wananchi kuongeza thamani ya mazao yao na
kuzalisha ajira.
Mhe.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 13 Juni, 2017 Ikulu Jijini Dar es
Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Waakuu wa Mikoa ya Tanzania Bara,
kikao ambacho kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George
Mcheche Masaju, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi na baadhi ya
Mawaziri.
Mhe.
Rais Magufuli amesema kila Mkuu wa Mkoa anapaswa kufanyia kazi fursa za
uanzishaji wa viwanda katika eneo lake na kuhakikisha anashawishi wawekezaji
kuzitumia fursa hizo kama inavyofanyika katika Mkoa wa Pwani ambako tangu Awamu
ya Tano iingie madarakani viwanda vikubwa 83 vimejengwa na vingine kukamilika
huku viwanda vidogo zaidi ya 120 pia vikiwa vimejengwa. Pamoja
na hilo Mhe. Rais Magufuli amewaagiza Wakuu wa Mikoa kuongeza juhudi za utatuzi
wa migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na kuharakisha mchakato wa kuwanyang’anya
hati za umiliki wa mashamba makubwa ambayo yanashikiliwa na watu pasipo
kuyaendeleza.
“Mashamba
yote yaliyotelekezwa, fuateni taratibu za sheria, yanyang’anyeni wapewe
Watanzania ambao wapo tayari kuyaendeleza, lakini fanyeni jambo hili kwa
kufuata utaratibu” amesema Mhe. Rais
Magufuli.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amewatahadharisha Wakuu wa Mikoa hao dhidi ya watu
wanaofanya njama za kujimilikisha maeneo makubwa ya ardhi na kusababisha wakulima
na wafugaji kukosa maeneo ya kilimo na malisho na ametaka wote watakaobainika
kufanya njama hizo wafichuliwe na kunyang’anywa maeneo hayo.
Mhe.
Dkt. Magufuli pia amewataka Wakuu wa Mikoa kushughulikia migogoro ya wakulima
na wafugaji na kuwahimiza wananchi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na
kuzalisha chakula cha kutosha katika maeneo yao.
Katika
kikao hicho Wakuu wa Mikoa wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa juhudi zake za
kuwapigania Watanzania hasa wanyonge na wamemuhakikishia kuwa wataendelea kumuunga
mkono katika juhudi hizo ikiwemo kudhibiti wizi wa rasilimali za Taifa kama
vile madini na maeneo ya hifadhi za wanyamapori.
Jaffar
Haniu
Comments