Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 26.04.2018


Mshambuliaji wa Liverpool Mohammed Salah
Image captionMshambuliaji wa Liverpool Mohammed Salah
Liverpool itazuia hamu yoyote kutoka kwa Real Madrid ya kutaka kumnunua mshambulaji wa Misri Mohamed Salah, ambaye wanasema ana thamani ya £200m. (Mail)
Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Roma Monchi ametetea uuzaji wa Salah kwa Liverpool, akisisitiza kuwa klabu hiyo ya Itali haikuwa na chaguo kutkana na matatizo ya kifedha.(Guardian)
Mkufunzi wa Real Madrid Diego Simeone
Image captionMkufunzi wa Real Madrid Diego Simeone
Mkufunzi wa Atletico Madrid Diego Simeone anasema kuwa hana mawasiliano yoyote na Arsenal kuhusu kazi ya ukufunzi ya klabu hiyo kufuatia tangazo la mkufunzi wake Arsene Wenger kwamba anaondoka mwisho wa msimu huu.Mirror)
Mkufunzi wa New York City Patrick Vieira angependelea kurudi Arsenal wakati mkufunzi Arsene Wenger atakapoondoka mwisho wa msimu huu na kuongezea kwamba yuko tayari kufunza Ulaya.(Times)
Mshambuliaji wa Wales na Real Madrid Gareth BaleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Wales Gareth Bale
Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale huenda akahamia Bayern Munich mwisho wa msimu huu , lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anasema kuwa lengo lake kuu ni kuisaidia Real Madrid kushinda mataji. (Bild, via Independent)
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amejiandaa kumuachilia mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 22, kuondoka mwisho wa msimu huu (Tuttosport, via Manchester Evening News)
Winga wa Man United Anthony MartialHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWinga wa Man United Anthony Martial
United inalenga kumshawishi beki wa klabu ya Fulham Ryan Sessegnon 17 kuhamia Old Trafford. (Times)
Arsenal huenda ikashindana na wapinzani wake katika ligi ya EPL Manchester United na Chelsea kwa usajili wa kiungo wa kati wa Roma na Ubelgiji mwenye umri wa miaka 29 Radja Nainggolan. (Sun)
Radja NainggolanHaki miliki ya pichaMARIO CARLINI / IGUANA PRESS
Image captionRadja Nainggolan
Manchester City na Manchester United zote zinamnyatia kiungo wa kati wa Napoli na Itali mwenye umri wa miaka 26-Jorginho. (Star)
Tottenham inataka kuwasajili wachezaji watatu wa Ureno mwisho wa msimu huu -winga wa Sporting Lisbon Gelson Martins, 22, beki wa kulia wa Southampton Cedric Soares, 26, na kiungo wa kati wa Wolves Ruben Neves, 21. (Mirror)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.