Manchester United
kwa mara nyingine wametangazwa kuwa klabu yenye thamani ya juu zaidi
Ulaya, ambapo thamani yao inakadiriwa kuwa €3.25bn (£2.9bn) kwa mujibu
wa kampuni ya KPMG.
Klabu hiyo ya England inaongoza kwa "thamani ya biashara", ikiwa mbele ya klabu nyingine kama vile Real Madrid na Barcelona.Orodha hiyo imeandaliwa baada ya utafiti uliofanywa kwa kuangazia taarifa za kifedha za misimu ya 2015-16 na 2016-17 ambapo waliangazia faida, haki za utangazaji, umaarufu, matarajio kutokana na uwezo wa kimichezo na thamani ya uwanja.
Liverpool, ambao wamefika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wamo nafasi ya nane kwenye orodha hiyo.
Kwenye utafiti huo ulioangazia klabu 32 kubwa, klabu za Ligi Kuu ya England zinajaza nafasi sita kati ya 10 za kwanza.
Andrea Sartori, mkuu wa michezo duniani katika KPMG ambaye ndiye mwandishi wa ripoti hiyo, anasema kwa jumla thamani ya klabu za soka imepanda katika mwaka uliopita.
- Manchester United wavuna zaidi ya Manchester City EPL
- Wenger: Sijui kama nitakutana na Mourinho tena
"Uhamisho wa wachezaji wa pesa nyingi pamoja na kuongezeka kwa mishahara hakujazuia klabu kuendelea kuongeza mapato, kwani faida kabla ya kutozwa ushuru uliongezeka kwa mara 17 ukilinganisha na mwaka uliotangulia."
Klabu 10 bora Ulaya kwa 'thamani ya biashara'
- Manchester United - €3.255bn
- Real Madrid - €2.92bn
- Barcelona - €2.78bn
- Bayern Munich - €2.55bn
- Manchester City - €2.16bn
- Arsenal - €2.10bn
- Chelsea - €1.76bn
- Liverpool - €1.58bn
- Juventus - €1.30bn
- Tottenham - €1.29bn
Kando na kutawala orodha ya 10 bora, kulikuwa na klabu nyingine tatu za Uingereza katika orodha ya 20 bora - West Ham United, Leicester City na Everton.
SSC Napoli (nafasi ya 17) nao wamekuwa klabu ya pili kwa thamani Italia, nyuma ya Juventus lakini mbele ya AC na Inter Milan.
Mwaka huu, klabu 12 zilikuwa na thamani ya zaidi ya euro bilioni moja, mbili zaidi ya 2017 ambapo zilikuwaklabu kumi pekee.
- Mambo muhimu yaliyotendeka siku ya mwisho Ligi Kuu England
- Wenger: Nitawakosa sana mashabiki wa Arsenal
- Sababu ya Ronaldo kuorodheshwa wa 49 duniani
- Jedwali la Msimamo wa ligi ya EPL 2017/18
Misimu ya 2015-16 na 2016-17, Manchester United walishinda Kombe la FA, Kombe la Ligi na Europa League. Lakini msimu huu wamemaliza bila kikombe hata kimoja.
Comments