KOCHA BENCHIKHA AMESEPA


 Baada ya kipigo cha Magoli (1-2) kutoka kwa Tanzania Prisons SC Kikiwa Kipigo cha Kwanza katika Mechi za Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara Tangu Ajiunge na Klabu hiyo, Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC Abdelihak Benchikha, leo Machi 7,2024 ameondoka nchini kuelekea nyumbani kwao nchini Algeria kwa ajili ya kushiriki kozi ya ya ukocha kwa siku tano huku akitaraiwa kurejea nchini kuendelea na majukumu yake baada ya siku chache.


Kocha Benchikha atakosa michezo miwili ya Ligi Kuu Bara, Mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Coastal Union utakaochezwa March 9, 2024 Jijini Tanga pamoja na mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Singida Foutane Gate FC utakaochezwa March 12 mwaka huu, Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo Ahmed Ally, amesema timu hiyo kwa sasa itakuwa chini ya Makocha wasaidizi Farid  pamoja na Suleiman Matola Kwa kipindi chote ambacho kocha mkuu Benchika hatokuwepo katika majukumu yake hadi pale atakaporejea nchini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI