RAIS SAMIA KUHUDHURIA IBADA MAALUMU YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 40 YA HAYATI SOKOINE

Msemaji wa Familia ya Hayati Sokoine, Kipuyo Lemblis alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dodoma Machi 28, 2024.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Zamaradi Kawawa akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Lemblis kuzungumza na wanahabari.
Sehemu ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kuhudhuria Ibada maalumu ya Kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Awamu mbili, Hayati Edward Moringe Sokoine aliyefariki kwa ajali ya gari mkoani Morogoro akitokea bungeni Dodoma kwenda Dar es Salaam Aprili 12, 1984.

Ibada hiyo itakayofanyika Aprili 12, mwaka huu imetangazwa na Msemaji wa Familia ya Hayati Sokoine, Kipuyo Lemblis alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dodoma Machi 28, 2024.

Lemblis amesema kuwa Ibada hiyo itakayofanyika Monduli Juu itahudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais Samia.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA










 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI