BALOZI NCHIMBI AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA NZUNDA SONGWE

 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, ameongoza maelfu ya waombolezaji wakiwemo viongozi na wananchi kutoka maeneo mnalimbali nchini, walioshiriki mazishi ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, marehemu Tixon Nzunda, yaliyofanyika huko Msinde, Kata ya Mpemba, Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe, Jumamosi Juni 22, 2024.

Marehemu Nzunda, ambaye hadi mauti yanamkuta kwa ajali ya gari Juni 18, 2024, akiwa ziara ya kikazi wilayani Hai, alikuwa mtumishi mwandamizi wa Serikali, akiwa amewahi kutumikia nafasi mbalimbali za utumishi wa umma, ikiwemo kuwa katibu mkuu wa wizara mbalimbali, baada ya kupanda ngazi za utumishi wa umma kutokea kuwa Ofisa wa Serikali ngazi ya wilaya.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

DEMU KAMA ANAFANYA KAZI HIZI KUWA MAKINI NAE.

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA