IJUE KWA UNDANI SHULE YA WASICHANA YA DK. SAMIA SULUHU HASSAN ILIYOFUNGULIWA NAMTUMBO

 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakifurahia picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, mapema  Septemba 27, 2024, baada ya Mhe. Dkt. Samia kuifungua rasmi shule hiyo iliyoko Namtumbo, mkoani Ruvuma. Shule hiyo ina uwezo wa kuchukua kwa mkupuo wanafunzi 1000.


Ujenzi wa shule hiyo, kwa mkoa wa Ruvuma, ambayo ni mojawapo kati ya shule 26 za wasichana zilizojengwa kila mkoa, ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025, ambao umewekewa msukumo mkubwa na Mhe. Rais Dkt. Samia, ndani ya miaka mitatu, tangu alipoingia madarakani. 


Hadi sasa Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia, kupitia Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP), ulioko chini ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ofisi ya Rais, imefanikisha ujenzi wa shule moja kwa kila mkoa nchini, kama ilivyoelekezwa na ilani hiyo ya CCM. 


Shule hiyo ya wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, inayoweza kuchukua wanafunzi takriban ya 1000 kwa mkupuo umegharimu kiasi cha Tsh. bilioni 4.6.


Hadi sasa shule hiyo iliyoko Kijiji cha Migelegele, Namtumbo, ina jumla ya wanafunzi 548, kati yao 420 wakiwa ni kidato cha tano na sita, na 128 ni kidato cha kwanza. Ina mabweni tisa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kila moja, huku kukiwa na bwalo la kulia chakula, linaloweza kuhudumia watu wapatao 1000 na pia kutumika kwa mikutano.


Rais Samia akivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Shule ya hiyo ya Sekondari ya Wasichana ya Mchepuo wa Sayansi na Sanaa ya Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Wakifurahi baada ya uzinduzi huo.
Muonekano kwa juu wa shule hiyo.
Rais Samia akihutubia wbaada ya kuizindua shule hiyo.
Katibu wa NEC wa Uchumi na Fedha, Dk. Frank Hawassi akitambulishwa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Shaibu akitambulishwa.
Moja ya mabango yenye ujumbe mwanana yaliyowekwa eneo hilo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi huo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

๐— ๐—•๐—ข๐—ช๐—˜ ๐—”๐—ฆ๐—œ๐—ง๐—œ๐—ฆ๐—›๐—” ๐— ๐—”๐—”๐—ก๐——๐—”๐— ๐—”๐—ก๐—ข ๐—ฌ๐—” ๐—–๐—›๐—”๐——๐—˜๐— ๐—” ๐—ฌ๐—” ๐—ง๐—”๐—ฅ๐—˜๐—›๐—˜ ๐Ÿฎ๐Ÿฏ.

DEMU KAMA ANAFANYA KAZI HIZI KUWA MAKINI NAE.

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA