UFUATILIAJI NA TATHIMINI IMEWEZESHA TARURA KUFIKIA MALENGO


 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.

Imeelezwa kwamba mpango mzuri wa ufuatiliaji na tathimini umewezesha Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kufikia malengo ambayo wamejiwekea katika kutekeleza dhima ya taasisi hiyo ya kujenga na kufanya matengenezo ya mtandao wa barabara za Wilaya nchini.

Akiongea kwenye Kongamano la Tatu la Kitaifa la Wiki ya Ufuatiliaji,Tathimini na mafunzo yanayoendelea kwenye hotel ya Golden Tulip, Zanzibar, Meneja Mipango wa TARURA Bw. Justin Lyatuu amesema kwamba namna ya kujua wamefikia lengo walilolipanga kwenye dira yao lazima wahusishe ufuatiliaji na tathimini.

“Kupitia ufuatiliaji ndipo tunafanya tathimini ili kuona kwanini hatufikii hatua na kama kuna kikwazo basi tunarudi nyuma kuangalia tatizo ni nini na hivyo tunaendelea kupima ili jamii iendelee kupata huduma za kijamii kwa kutumia barabara”.

Amesema Kongamano hilo linawaongezea uelewa kwani wao kama TARURA kwa matengenezo ya barabara lengo lao ni kuwaunganisha wananchi kwa kupita kwenye barabara nzuri.

Nao baadhi ya washiriki wa kongamano hilo ambalo wametembelea banda la TARURA wamepongeza Wakala kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kufungua barabara za wilaya na hivyo kuwasaidia wananchi kuinuka kiuchumi kwakuwa hivi sasa wanaweza kusafirisha mazao yao kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CPA MAKALLA 'KUUTEKA' MKOA WA ARUSHA

ASKOFU CHANDE AISHUKURU SERIKALI KULIPATIA USAJILI WA KUDUMU KANISA LA KARMELI

DEMU KAMA ANAFANYA KAZI HIZI KUWA MAKINI NAE.

JENGENI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA NJOMBE-MWANYIKA

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA