WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS SAMIA UNGA79*


 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Alhamisi, Septemba 19, 2024) kwenda Marekani ambako atamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA79).


Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 20-26, 2024, utafanyika jijini New York, Marekani ambapo masuala ya kiuchumi, biashara, nishati, siasa, mazingira, afya, vijana na watoto yatajadiliwa. Masuala mengine ni ya maji, bahari, athari za hali ya hewa na haki za binadamu.


Katika mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka, viongozi wa nchi mbalimbali wanatarajiwa kushiriki mijadala tofauti chini ya mada kuu ambayo ni “Hakuna kuachwa nyuma yeyote: Kushirikiana pamoja kuendeleza amani, maendeleo endelevu na heshima ya binadamu kwa vizazi vya sasa na vijavyo" (Leaving no one behind: Acting together for the advancement of peace, sustainable development and human dignity for present and future generations).


Mbali na kukuza diplomasia, ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano huo unatoa fursa ya nchi kuwasilisha maslahi yake katika jukwaa la kimataifa, kujifunza kutokana na uzoefu wa nchi nyingine na pia kuwasilisha ajenda na mipango ya maendeleo ya nchi kwa jamii ya kimataifa.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CPA MAKALLA 'KUUTEKA' MKOA WA ARUSHA

ASKOFU CHANDE AISHUKURU SERIKALI KULIPATIA USAJILI WA KUDUMU KANISA LA KARMELI

DEMU KAMA ANAFANYA KAZI HIZI KUWA MAKINI NAE.

JENGENI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA NJOMBE-MWANYIKA

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA