SERIKALI YASHUSHA MAAGIZO KWA WATHIBITI UBORA WA SHULE


 NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Mahera,akizungumza wakati akifunga Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule  yanayofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule Ephraim Simbeye,akiipongeza Wizara ya Elimu kwa kuandaa Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule  yanayofanyika jijini Dodoma.

BAADHI ya washiriki wakimsikiliza Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Mahera,(hayupo pichani) wakati akifunga Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule  yanayofanyika jijini Dodoma.

 NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Mahera,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga  Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule  yanayofanyika jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna_ Dodoma

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Mahera,amewataka Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule nchini kuzingatia sheria, kanuni, miongozi na taratibu katika usimamizi na utekelezaji majukumu yao.

Dkt.Mahera ametoa Maelekezo hayo jijini Dodoma, wakati akifunga Mafunzo Elekezi ya siku tatu kwa Maofisa Uthibiti ubora wa Wilaya Wateule ikiongozwa “Kaulimbiu inayosema Uthibiti Ubora wa Shule unaozingatia Weledi, Maadili na Uwajibikaji kwa matokeo chanya ya ujifunzaji”

Dkt.Mahera, amezitaka taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo kutekeleza maelekezo ya Serikali kwa kufanya kazi Kisekta ili kuweza kuwa na matokeo makubwa katika Mageuzi ya elimu nchini.

” Ukitaka kufanikiwa katika Sekta hii ya elimu ni lazima uhakikishe unafanya kazi Kisekta yaani kwa kushirikiana na Idara za elimu na sekta nyingine ambayo inatoa elimu na hayo ndio maelekezo ya Serikali ili kupata matokeo Makubwa katika Ubora wa Elimu na sio lazima kufanya kazi kama Wizara,” ameeleza Mahera

Dkt. Mahera amewataka Wathibiti Ubora hao kuhakikisha wanatumia fedha kidogo walizonazo kuleta matokeo kwani Serikali inategemea matokeo zaidi kutoka kwao.

” ukifanya kazi nzuri hata hao unaowafanyia watakufurahia na maendeleo yako yataonekana kwani kila mmoja atakuwa an Ashuhudia, hata zikitokea nafasi za Juu unaweza ukajumuishwa na hayo ndio matunda ya kuwatumikia vyema wananchi na nafasi uliyekasimiwa kikamilifu,

“Nimefahamishwa kwamba mmejifunza mambo mengi katika mafunzo haya ambayo ni pamoja na; Wajibu wenu katika usimamizi wa utekelezaji wa Mitaala iliyoboreshwa; Maeneo muhimu ya Kiunzi cha Uthibiti Ubora wa Shule yaliyoboreshwa kulingana na mabadiliko yanayoendelea katika sekta ya Elimu; Mfumo wa uthibiti ubora wa Shule, muundo wake na namna utakavyotumika pale utakapokuwa tayari; taratibu za manunuzi ya Umma kwa kutumia mfumo wa NeST,

“Aidha, nimefahamishwa pia mmejadili kuhusu matumizi ya mfumo wa usajili wa shule (SAS), masuala ya taratibu za fedha, masuala ya Sheria ya Elimu na yahusuyo utawala na uendeshaji wa ofisi zenu. Ni matumaini yangu kuwa mlitumia muda wenu vizuri na nategemea maarifa na stadi mlizojifunza zitawapatia weledi katika kuzifanya kazi zenu na kuwa chachu ya kuongeza uwajibikaji,”ameeleza Mahera

Dkt. Mahera amesema Uthibiti Ubora wa Shule ni chombo muhimu cha kutathmini ufanisi wa shule na vyuo vya ualimu katika mchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji.

Hivyo, Wajibu huo unawataka wathibiti ubora kuzisaidia Taasisi wnazozifanyia tathmini ili ziweze kufikia viwango vya Ubora vilivyowekwa na nchi. Hivyo, ni muhimu sana kujiongezea ujuzi na maarifa kila wakati pengine pasipo kusubiri mafunzo kama hayo kutokana na upatikanaji wa rasilimali fedha.

“Ni vema kuwa na jitihada binafsi za kujiongezea maarifa kupitia fursa nyingine za kutumia kwa manufaa maendeleo ya Sayansi na Teknolojia duniani na ya mitandao mbalimbali,” amesisitiza Dkt. Mahera

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule Ephraim Simbeye amesema Wizara ya Elimu kupitia Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule, imefanikiwa kutekelezaji maboresho ya Muundo wa Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule ambapo kwa sasa muundo unawatambua Maafisa Uthibiti Ubora wa Wilaya, cheo chenye majukumu ya waliokuwa Wathibiti Wakuu Ubora wa Shule (W1)

“Kufuatia maboresho ya Mitaala ya Elimumsingi, Wizara imeboresha Kiunzi cha Uthibiti Ubora wa Shule cha Mwaka 2017 na Miongozo yake ili viendane na matakwa ya mitaala ,” amesema Simbeye

Pia Simbeye amewataka wathibiti ubora nchini kulinda miundombinu na rasilimali walizokabidhiwa ili ziweze kuwasaidia katika kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza katika utendaji kazi wao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO SABA AMBAYO WANAUME WENGI HAWAYAPENDI:

NI HESHIMA KUBWA SANA KUIFUNDISHA YANGA - KOCHA MPYA WA YANGA

”RAIS SAMIA AUMIZWA MAUAJI YA KIBIKI”

UOKOAJI KARIAKOO NI USHUHUDA WA MOYO WA UTANZANIA: NCHIMBI

KOCHA SEAD RAMOVIC AMRITHI GAMONDI YANGA.

TAMISEMI PUUZENI DOSARI NDOGONDOGO ZA WAGOMBEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA - DK. NCHIMBI

CCM YASAMBAZA VIONGOZI NA MAKADA WAANDAMIZI NCHI NZIMA

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE