Meneja Habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally ametumiwa barua ya madai kutoka Yanga Sc inayomtaka kuilipa klabu ya Yanga Sc kitita cha BILLION 10 za Kitanzania kutokana na makosa mawili ya kuzungumzia mkataba wa kiungo Pacome Zouzoua pamoja na tuhuma za ushirikina.
Kuhusu mchezaji Pacome Zouzoua Ahmed Ally amedaiwa kusema mchezaji huyo anamaliza kandarasi yake ndani ya Yanga na Simba wanatazama namna ya kumsajili na kuna kauli za ukakasi alizungumza ambazo zimeharibu ‘brand’ ya Yanga kwa wabia wake ikielezea kuwa alitaja mpaka mambo ya sindano.
Kauli ya Ahmed kuhusu Pacome imesema: “Pacome amemaliza mkataba tukiona anafaa tutahangaika nae, Pacome amemaliza mkataba ndani ya Yanga na hana mpango wa kuongeza .mtanyoa ndevu mwaka huu hana mpango wa kuongeza amechoka kuchomwa sindano kila siku kama anazuia mimba”
“Tunaangalia kiwango chake kama kitaturidhisha tutahangaika nae lakini kama ataendelea na mwenendo wake anaoendelea nao tutawaachia...kama tulivyowaachia Chama na tunataja majina Live hakuna kutumia code”
Aidha kuhusu tuhuma za uchawi Ahmed Ally ametakiwa kuthibitisha nj namna gani Yanga ni Wachawi kwa maana hawajawahi kupewa adhabu yoyote na Bodi kuhusu Uchawi.
Yanga wanamtaka Ahmed afanye yafuatayo ndani ya siku tano (5)
1. Kuomba radhi kwa njia sawa na aliyotumia kutoa kauli yake.
2.Kufidia malipo ya Tsh Bilioni 10 (10,000,000,000) Yanga wamemaliza kwa kusema kama hayo maagizi hayatafanyiwa kazi watafuata hatua za kisheria zaidi.
#KitengeSports
Comments