MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa Treni ya SGR imepata mafanikio makubwa kwa kusafirisha zaidi ya abiria 1.5 tangu ianze Agosti mwaka jana.
Pamoja na mambo mengine, ameyasema hayo mbele ya vyombo vya habari katika Stesheni ya Mama Samia, Mkonze jijini Dodoma, akijiandaa kusafiri na Treni hiyo kuelekea Morogoro.
Aidha, Msigwa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Utamadu I, Sanaa na Michezo, amesema kuwa sasa serikali imeshaingiza nchini mabehewa ya mizigo 264 na tayari imeagiza mabehewa mengine 264. Treni hilo likianza litakuwa na uwezo wa kusafirisha Tani 10,000 kwa wakati mmoja.Msigwa akizungumza na waandishi wa habari katika Stesheni ya Treni ya SGR, ya Mama Samia Dodoma.
Baadhi ya abiria wakiwa wameshuka kutoka kwenye treni hiy.
Baadhi ya abiria wakiwa wameshuka kutoka kwenye treni hiy.
Comments