KAMATI YA BUNGE YAWAPA TANO OFISI YA WAZIRI MKUU KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU.





Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeridhishwa na utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa namna inavyowagusa wananchi, huku ikimpongeza Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kukuza ustawi na maendeleo ya Watanzania.


Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Fatuma Toufiq, leo Januari 21, 2025, jijini Dodoma wakati ikipokea taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2024.


Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, amesema ofisi hiyo katika mwaka wa fedha 2024/2025 imepanga kuendelea kutekeleza shughuli mbalimbali, zikiwemo usimamizi wa kazi na huduma za ukaguzi, maendeleo ya vijana, kuratibu shughuli za ajira, utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu, hifadhi ya jamii, na ukuzaji wa tija. Ameahidi kuwa ofisi hiyo itatekeleza majukumu hayo kikamilifu ili kufanikisha malengo yaliyowekwa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA