KAMPUNI YA SIMBA BINGWA INATARAJIA KULETA MELI MOJA YENYE SHEHENA YA MIZINGO KUPITIA BANDARI YA TANGA

 


Na Ashrack Miraji 

KAMPUNI ya Simba Bingwa kupitia Simba Supply chain solutions ltd (SSCS) chini ya kampuni yake tanzu Simba Terminal katika mwaka huu wa 2025 inatarajia kila baada ya miezi mwili hadi mitatu kuleta Meli moja yenye shehena ya mzigo kupitia Bandari ya Tanga.

Taarifa hiyo imetolewa na Awadh Massawe, Meneja wa Kampuni hiyo, aliyesema kwamba, Simba Terminals chini ya jitihada kubwa za wakurugenzi na bodi yake wamefanikiwa kufanya ushawishi kwa Wateja wao wa ndani na nje ya nchi kuitumia Bandari ya Tanga.

Januari 19 ,2025 Simba Terminals imepokea meli ya MV WL UGLICH iliyokuwa na tani 7,000 za shehena ya mzigo wa Nitrate kutoka Russia, bidhaa ambayo ameahidi wataweza kuipakuwa na kuisafirisha kwa Wateja wao kwa ufanisi mkubwa.

Ujio wa Meli hiyo umetimiza idadi ya meli tisa tangu Simba Terminals kuanzia kutumia Bandari ya Tanga, ambapo Massawe anasema, kwa kiasi kikubwa Wateja wake wameridhishwa na maboresho yaliyofanyika ikiwa ni pamoja na utendaji hatua ambayo imewasababisha kuoneaha utayari wa kuendelea kuitumia Bandari ya Tanga.

"Meli imepakia tani 7,000 za nitrate tutapakua na kuisafirisha kwa ufanisi kwenda kwa Wateja wetu ndani na nje ya Tanzania, tunayo magari 700 hadi 800" anasema Massawe.

Aidha Massawe amesema, kampuni imefanya jitihada mbalimbali za kununua Vifaa na hapa anataja mashine zinazowawezesha kuhakikisha bidhaa zinawekwa kwenye utaratibu mzuri kabla ya kuwafikia Wateja wao.

Pamoja na hayo, Massawe amesema, ufanisi katika Bandari ya Tanga umeendelea kuwa mkubwa ikilinganishwa na Bandari nyingine za jirani hatua ambayo imetoa fursa kubwa kwao kuendelea kuwashawishi Wateja wao wa ndani na nje ya nchi kuitumia Bandari ya Tanga.

Hayo yote ni matokeo ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyewekeza zaidi ya Shilingi Bil 429 ili kufanyika kwa maboresho likiwemo suala la kuongeza kina kwenye Bandari ya Tanga

Mambo mengine ambayo Massawe anayaona kuwa yamechangia upatikanaji wa mafanikio, ni pamoja na mshikamano uliopo baina yao na Mamlaka zote zinazohusika na utendaji kupitia Bandari ya Tanga.

Na hapa Massawe anatoa wito kwa Wateja wao wa ndani na hata wale wa nje ya nchi kama DRC, Zambia na nyinginezo kuendelea kuhamasika katika kutumia Bandari ya Tanga ili kunufaika na upatikanaji wa huduma bora kulingana na uwekezaji uliofanyika.

Kupitia uwekezaji mradi mkubwa wa maboresho ya kuongezwa kuna kwenye Bandari ya Tanga, mapato ya Serikali yataongezeka huku kipato kwa mwananchi mmoja mmoja kikiendelea kuimarika.

Massawe ameendelea kutoa Wito kwa Wadau wengine kuona umuhimu wa kuitumia Bandari ya Tanga huku akiishauri Serikali kufanya jitihada za kuongeza uwekezaji kwa kupanua zaidi sehemu ya kuweza kuhifadhia mizigo.





 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA