1. Wanawake wana uwezo wa kihisia wa asili ndani yao wakati wanaume wanatumia akili zaidi. Kila jambo lazima liwe na maana kwa wanaume. Matumizi ya hisia yanaweza yasiwe sahihi muda wote, mkeo anaweza asiweze kukuelezea sababu za kwanini anashauri ama anapendelea jambo fulani, lakini usipotezee anachokisema. Hivyo jifunze KUMSIKILIZA mkeo.
2. Unatakiwa kulinda eneo lililoko ndani ya mipaka yako kama mwanaume. Wanaume huwa wanamiliki maeneo yao kikawaida na kwa muktadha huu, eneo lako ni mkeo. Mlinde, usimuache bila ulinzi na gharamia mahitaji yake.
3. Kama wewe ni mwanamke, mumeo siyo "mwamke mwenzio". Kama wewe ni mwanaume, mkeo sio "mwanaume mwenzako". Usihusiane na mwenzako kama mtu anayehusiana na mtu wa jinsia yake. Mkeo siyo "msela wako".
4. Mkeo anapozungumza, wakati mwingine hataki utoe suluhu yoyote. Anataka tu kuzungumza. Hivyo usimkatishe wakati anapokusemesha, wewe furahia mazungumzo tu.
5. Kama wewe ni mwanaume na hauishi maisha ya kiroho uko kwenye nafasi hatari sana. Usiache jukumu la maombi na kiroho kwa mkeo pekee. Mtakuwa na maendeleo mengi zaidi kwenye familia yenu ikiwa mtazipa kipaumbele kanuni za Mungu nyumbani mwenu.
Asante kwa kusoma na kushea ππΏππΏππΏ
Comments