Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi ameteuliwa kuwa Mgombea Mwenza wa kiti cha urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotariwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Jina la Dk. Nchimbi liliwasilishwa katika mkutano mkuu na mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia amepitishwa na wajumbe wa mkutano huo kuwa Mgombea urais mteule wa chama hicho katika uchaguzi huo.
Katika mkutano huo wajumbe wamethibitisha jina la Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM
Comments