RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AAWANYOOSHEA NJIA YA URAIS WA DK.SAMIA NA DK.MWINYI 2025

 *Ashauri liandikwe Azimio kisha lipitishwe na Mkutano Mkuu

Maalum

*Wajumbe wote wasema wanakwenda na Rais Samia,wanakwenda na Dk. Rais Mwinyi

-Dodoma

RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete ameonyoosha ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan pamoja na Dk.Hussein Ali Mwinyi majina yao kupitishwa na Mkutano Mkuu maalum kugombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Kikwete ametoa ushauri huo leo katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Dk.Samia Suluhu Hassan.

Kabla ya Rais mstaafu Kikwete kutoa maelezo na ushauri wake kuhusu majina ya viongozi hao kupitishwa kugombea urais wajumbe wa mkutano mkuu Maalum walitoa mapendekezo kuwa kazi ambayo viongozi hao wameifanya ni vema mkutano huo ukapitisha rasmi majina yao.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama hicho aliyekuwa akiongoza kikao pamoja na kusikia maoni ya wajumbe,alimuomba Rais mstaafu Kikwete kutoa ushauri wake.

“Tumsikiliza taarifa za utekelezaji wa Ilani ,uwepo wenu Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na Rais Dk.Hussein Mwinyi mnajua Mnakokwenda,yameelezwa mengi mazuri.Kwa mambo ambayo yamefanyika ushindi kwa Chama Cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu mwaka 2025 hauna shaka hata kidogo.

“Kuhusu la wajumbe ajenda ya kwanza ilikuwa ni kupokea utekelezaji lakini hii rai ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na Dk.Hussein Ali Mwinyi kupitishwa na mkutano mkuu maalum limesemwa na wajumbe wa mkutano huu Mkuu Maalum

“Kila chama kina wakati wake wa kuteua wagombea na kama tunataka leo tuamue leo kama Samia ndio mgombea wetu na Dk.Hussein Mwinyi ndio mgombea wetu mamlaka hayo tunayo.

“Yanapozungumza mambo makubwa mnatulia kusikiliza na baada ya hapo ndio tunatoka na
Mabango.Tukiamua ndio tumeamua na yanayobakia ni masuala ya kisheria tu.Hivyo kwa maana nyingine tayari wanaondoka wanafahamu nini tumekuamua.

“Kama tumekubaliana katika mkutano huu ndio tumeshakubaliana ,Rais Samia mitano tena,Rais Mwinyi mitano tena,”amesema Kikwete alipokuwa akitoa ushauri wake kuhusu hoja ya wajumbe.

Hata hivyo Rais mstaafu Kikwete ameshauri kuandikwa azimio na wajumbe wa mkutano huo wapitishe na wakubali hapo ndio itakuwa sawa

“Hapa lipitishwe Azimio na likubaliwe hapo sawa, tukifanya hivyo ndio itakuwa rasmi sio kuongea tu,Azimio liseme kabisa kuwa tumemteua Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kugombea urais kwa tiketi ya Chama hicho…

“Tuandike azimio kuwa Dk.Hussein Ali Mwinyi amepitishwa kaouwa mgombea wetu wa urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu kwa mgombea urais katika uchaguzi.Tukifanya hivyo tutakuwa rasmi.”

Baada ya maelezo hayo Rais mstaafu Kikwete alianzisha wimbo unaosema
“Tunaimaaaani na Samia…tunaimani na Dk.Hussein Ali Mwinyi” Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wote wakawa wanaimba na shangwe wakati wote lilikuwa limetawala.Kwa hisani ya 
Said Mwishehe



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA