Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21, lina Sekondari za Kata 26 na 2 za Binafsi. Sekondari mpya 6 zimepagwa kufunguliwa mwaka huu. Matayarisho ya kuanza ujenzi wa sekondari nyingine sita (6) yamekamilika.
Muhoji Sekondari inajengwa Kijijini Muhoji, Kata ya Bugwema. Hii ni sekondari ya pili ya kata hii.
Muhoji Sekondari ilianza kujengwa kwa kutumia michango ya Wanakijiji, Mbunge wa Jimbo la MusomaVijijini, na baadhi ya Wazaliwa wa Kijiji cha Muhoji. Serikali Kuu imeanza kuchangia ujenzi wa sekondari hii kwa kutoka Tsh milioni 75.
Miundombinu ya elimu ya awali imekamilishwa:
Muhoji Sekondari iko tayari kupokea wanafunzi wa Kidato cha Kwanza (Form I) - ukamilishwaji umefanywa kwenye vyumba vya madarasa, ofisi za walimu, vyoo, maktaba na chumba cha matibabu
Wazazi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, kwenye Kikao chao cha leo, wamekubaliana yafuatayo:
(i) Wazazi watachangia upatikanaji wa chakula cha mchana kwa wanafunzi wote
(ii) Wazazi watanunua madawati ya watoto wao. Madawati yanatengenezwa kijijini hapo
(iii) Wazazi watahakikisha kuna uhusiano mzuri kati yao (Wazazi) na Walimu, na kati ya Wanafunzi na Walimu
(iv) Wazazi wataendelea kushirikiana vizuri na Serikali kuhakikisha Sekondari yao inatoa elimu kwenye mazingira mazuri yenye mafanikio mazuri.
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
Matayarisho ya ufunguzi wa Muhoji Sekondari ya Kijijini Muhoji, Kata ya Bugwema, Musoma Vijijini
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumatano, 15 Jan 2025
Comments