USIA WA BABA KWA BINTI YAKE ANAYE OLEWA.....

1) Mwanangu unakwenda kuolewa na Mwanaume (Mume) na siyo marafiki, Hakikisha haushindi kwa Marafiki sasa kama ilivyokuwa kabla ya kuolewa kwako, Umesikia Mwanangu.....Heshimu ndoa yako,
2) Mwanangu SIRI ZAKO NA MUMEO ni MARUFUKU kuzitoa nje, Usifikiri kila unayemuelezea SIRI Zako na za Mumeo anafurahia WENGINE wanakucheka, JIFUNZE KUTUNZA SIRI ZAKO NA MUMEO Mwanangu...,
3) Mwanangu Wewe ni Mlinzi wa MUMEO...Mlinde kwa MAOMBI Kila WAKATI Usifikiri MAOMBI YAMEISHA ULIPOINGIA KWENYE NDOA, HAPANA UKIZUBAA TU UTANYANG'ANYWA MUMEO NA WIZI WA WAUME ZA WATU.
4) Mwanangu Mimi na Mama Yako tumezeeka na muda wetu umetutupa mkono ila furaha yetu inaenda kutimia kwa kukulea, ukakua katika maadili na ndoa yetu sasa na wewe unaenda kupata yako tumetimiza ndoto yetu ya kukuona ukiwa mama ambaye atakae enzi yote mema na kuwa na ndoa itakayodumu kama yetu ikitawaliwa na furaha na upendo... Linda sana ndoa yako.
5) Mwanangu ulipokua mdogo shuleni na nyumbani tulikusifu sana kuwa umechangamka na wajua kuongea kweli kweli tena umerithi kutoka kwa bibi yako ila mwanangu mdomo ule umezibwa rasmi leo yakupasa kuwa na maneno machache au ukimya kabisaa maana katika ndoa uongeaji saaaaana ni kero kubwa .... Cha msingi msikilize mumeo.
6) Mwanangu leo unaolewa na mumeo mtakayeishi pamoja milele siyo mwanasiasa au mshindani wa debate shuleni, tafadhali epuka argument au mabishano yasiyo na msingi ili kujenga familia yenye furaha muda wote... mabishano ni sumu katika ndoa.
7) Mwanangu unaolewa, kule unakoenda kuishi tambua siyo kituo cha redio au television bali ni nyumbani kwako wewe na familia yako, hivyo ni marufuku kupokea au kusambaza habari za ndani na nje... Epuka umbea ni uchafu katika ndoa.
😎 Mwanangu siku ulipojisikia kuumwa au shida yeyote mtu wa kwanza kumshirikisha alikua mama yako kisha baadae mimi, hakika ulifanya vyema kabisaaa ila sasa mwanangu kuanzia leo ikitokea jambo lolote mtu wa kwanza kumshirikisha awe mme wako.... muamini mumeo.
9) Mwanangu tumekufunza yote ila hatujakufunza mafunzo ya kivita na uasi tafadhali tambua kule unakoenda kuishi mmeo ana wazazi na ndugu zake, waheshimu kama ulivyokua unatuheshimu, dumisha upendo tambua wao sasa ndio familia yako mpya.... Epuka kuwa mchochezi na chanzo cha migogoro na chuki, NDOA ISIJE IKAKUSHINDA.
10) Mwanangu siku zote amini chochote apatacho mumeo ni majaaliwa ya MUNGU usitamani maisha ya wengine, mvumilie mmeo kwa chochote alichonacho au apatacho,
ridhika nae, mkumbatie mtie moyo muombee hakika mtafanikiwa ardhini na mbinguni maana MUNGU hujibu maombi yao wamtafutao kwa bidii wakizishika amri zake na kujituma katika kufanya kazi.. Epuka mafundisho ya kitchen part ya kusafisha KINU, MWIKO na kumuweka mmeo ndondocha kisa tamaa ya utajiri na mali nyingi.

May be an image of 1 person
All reactions:
6





 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA