Mwenyekiti wa Kamat ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Fatma Toufiq (kushoto) akiongoza kikao cha kukusanya maoni kutoka kwa wadau kuhusu muswada wa sheria wa marekebisho ya sheria ya kazi ya mwaka 2024 katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa Lounge, Dodoma Januari 15, 2025.
Mwanasheria wa Chama cha Wafanyakazi wa Malori Tanzania (CHAWAMATA), Alfred Louis akitoa maoni ya chama hicho kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kuhusu muswada wa sheria wa marekebisho ya sheria ya kazi ya mwaka 2024 katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa Lounge, Dodoma Januari 15, 2025.
Baadhi ya mambo aliyopendekeza ni;
Kutetea Kifungu cha 40(1)(c) Kwenye Sheria ya Ajira na mahusiano kazini ibaki kama ilivyokuwa mwanzo
kuhusu mabadiliko ya kifungu cha 40(1)(c) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, ambayo yanapendekeza kwamba mfanyakazi anayefutwa kazi bila sababu halali au bila kufuata utaratibu halali atalipwa fidia ya mishahara isiyozidi miezi 12, badala ya kima cha chini cha mishahara isipungue miezi 12, kama ilivyokuwa awali.
Baadhi ya wadau wakitoa maoni yao.
Mmoja wa wadau akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kuhusu muswada wa sheria ya usimamizi wa mazingira wakati wa kikao cha kukusanya maoni ya wadau.
Baadhi ya wadau wakiwa katika kikao hicho.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Anna Lupembe (kushoto) akiongoza kikao hicho.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAKENDA
0754264203
Comments