ZAIDI YA 200, 000 WAOMBA AJIRA YA UALIMU

Zaidi ya Watanzania 200,000 wameomba ajira ya ualimu kuwania nafasi 14,000 zilizotangazwa na Sekretarieti ya Ajira baada ya kibali kutolewa na Rais.


Idadi hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika Mji wa Kiserikali Mtumba, jijini Dodoma Januari 11,2025.


Katika kuwapunguzia gharama, Simbachawene amesema kuwa waombaji wote watafanyiwa usaili katika katika mikoa waliyoombea kazi hiyo ambapo watatakiwa kuwa na vyeti vya taaluma na cheti cha kuzaliwa pamoja na kuwa na moja ya vitambulisho vifuatavyo; Kitambulisho cha Nida, cha mpiga kura, leseni ya udereva, hati ya kusafiria, kitambulisho cha kazi na cha ukaazi au barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa, Kijiji.


Waziri Simbachawene,amebainisha kuwa asilimia kubwa ya walimu hao watakuwa ni wenye taaluma ya amali yaani ufundi waliofuzu kutoka vyuo mbalimbali vya ufundi na kwamba kabla ya kuanza kazi watapatiwa mafunzo maalumu ya ualimu.


Ametaja aina tatu za usaili zitakazotumika ambazo ni; wa kuandika, usaili wa vitendo na usaili wa mahojiano wa ana kwa ana.


Waziri Simbachawene akizungumza na vyombo vya habari,

 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA

DK. KIKWETE AZINDUA KITUO CHA AFYA KIZIMKAZI, APONGEZA MAENDELEO ZANZIBAR

KOCHA WA MAMELODI ASIMAMISHWA KWA KUWAPIGA CHABO WACHEZAJI WAKE WA KIKE