NHIF SACCOS YAJISUKA UPYA

 Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu Dkt. David Mwenesano ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu Dkt. Irene Isaka, akiwapongeza wanachama wa Bima ya Afya Saccos kwa kuwa ndani ya SACCOS ambayo inawawezesha kifedha.

Mwenyekiti wa NHIF SACCOS Bw. Abdallah Jumatatu akiwahakikishia wanachama wa Saccos hiyo kuwa uongozi umejipanga na kuweka mikakati ya kulinda uhai wa Chama hicho kwa kuwa na mtaji imara utakaowawezesha wanachama kuboresha maisha yao.






 

Mwenyekiti wa NHIF SACCOS Bw. Abdallah Jumatatu amewahakikishia wanachama kuwa uongozi umejipanga na kuweka mikakati ya kulinda uhai wa Chama hicho kwa kuwa na mtaji imara utakaowawezesha wanachama kuboresha maisha yao.


Hayo ameyasema jana wakati akiwasilisha taarifa ya SACCOS hiyo mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wanaotoka katika Ofisi zote za Mfuko nchini.


Alisema kuwa dhamira kuu ya uongozi uliopo madarakani ni kuona wana SACCOS hao wakiboresha maisha yao kupitia michango wanayochangia lakini pia kupata fedha za maendelea pale wanapokuwa wakizihitaji.


"Tunafahamu tuna muda mfupi tangu mtuchague lakini jambo kubwa ambalo tumelisimamia kwa nguvu zote ni kuhakikisha mwanachama hakosi fedha wakati anapohitaji na huo ndio uimara tunaoutaka, tunaomba tushirikiane kwa pamona ili wote tuweze kufikia maendeleo tunayoyatamani, niwaombe sana nanyi pia tuweke kipambaule katika uwekaji wa hisa unaoimarisha zaidi SACCOS yetu," alisema Bw. Jumatatu.


Alitumia fursa hiyo pia kuwaomba wajumbe hao kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya ili wawe na uhakika wa kupata huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha.


Naye Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu Dkt. David Mwenesano ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu Dkt. Irene Isaka, aliwapongeza watumishi hao kwa kuwa ndani ya SACCOS ambayo inawawezesha kifedha.


"Niwapongeze sana kwa uamuzi wa kuwa wanachama, hii inaonesha mna nidhamu ya fedha kwa kuwa mnaweza kukopa na kurejesha, hii pia inasaidia kuleta ufanisi mahala pa kazi kwa kuwa mnapohitaji fedha mnazipata kupitia SACCOS yenu nawapongeza sana" alisema.


Kwa upande wa wajumbe wamefurahishwa na usimamizi imara wa fedha unaofanywa na viongozi waliopo madarakani.


*Bima ya Afya kwa Wote,Jiunge Sasa*

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA

NOTI MPYA KUANZA KUSAMBAZWA MWEZI UJAO

HUYU NDIYE DKT. NCHIMBI, MAKAMU WA RAIS AJAE

CHAKUHAWATA WANENA MAKUBWA--