Manchester United wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Tottenham mwenye umri wa miaka 32 kutoka Korea Kusini Son Heung-min. (Fichajes)
Wachezaji wapya wa MLS San Diego FC wanakaribia kukubali dili la kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, kwa uhamisho wa bure wakati kandarasi yake ya Manchester City itakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (TBR Football)
Real Madrid wanatazamiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnunua beki wa kati wa RB Leipzig, 22, Castello Lukeba, ambaye pia anavutiwa na Liverpool, Chelsea na Manchester United. (Mirror)
Nottingham Forest, Newcastle United na Everton wanamfuatilia mshambuliaji wa Marseille wa Brazil Luis Henrique, 23. (TBR Football)
Juventus wanataka kumsajili mlinzi wa Feyenoord mwenye umri wa miaka 27 kutoka Slovakia David Hancko, ambaye ana nia ya kutaka kuhamia Turin licha ya kuwindwa na Liverpool. (Tuttosport )
Barcelona wamempa mshambuliaji wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28 na Colombia Luis Diaz kipaumbele cha uhamisho msimu huu. (Diario AS)
Chelsea wanalenga beki wa Ufaransa Loic Bade kutoka Sevilla katika majira ya joto. The Blues wanasemekana kuwa tayari kutoa dau la euro 30m (£24.9m) kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Fichajes)
Comments