UMEME NA USTAWI WA KISIWA CHA RUKUBA CHA MUSOMA VIJIJINI*


 *

1. Kituo cha Afya cha Kisiwa cha Rukuba kimefungiwa umemejua (solar energy) wa thamani ya Tsh 345,600,000 (Tsh 345.6m)


2. Sehemu nyingine za Kisiwa hicho zitafungiwa umemejua (solar energy) kupitia Mradi mkubwa wa kufungia umemejua kwenye Visiwa vya nchi nzima vilivyoko Bahari ya Indi na Maziwa yetu makuu.


        Kwa hiyo, Kisiwa cha Rukuba nacho kiko ndani ya Mradi ambao matayarisho yake yanakamilishwa (Taarifa kutoka REA kwenda kwa Mbunge wa Jimbo)


*Maji ya bomba Kisiwani:*

Baada ya umemejua kusambazwa Kisiwani Rukuba, RUWASA itaendelea na mradi wake wa kusambaza maji ya bomba Kisiwani humo


*Elimu Kisiwani:*

Kisiwa cha Rukuba kina Shule ya Msingi yenye Maktaba na nyumba za makazi ya walimu wote. Upungufu wa vyumba vya madarasa haupo!


Sekondari mpya inajengwa Kisiwani humo, na imepangwa ifunguiliwe mwaka huu, 2025.


*Huduma za Afya Kisiwani:*

Kituo cha Afya kimeanza kutoa huduma za matibabu. Kituo hiki kimefungiwa umemejua (solar energy)


*Picha iliyoambatanishwa hapa inaonesha:*

Miundombinu ya Umemejua (solar energy) iliyofungwa kwenye Kituo cha Afya cha Kisiwa cha Rukuba cha Musoma Vijijini.


*SHUKRANI:*

Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba na Viongozi wao wa ngazi mbalimbali wanaendelea kuishukuru sana Serikali yetu, chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo ya Kisiwa cha Rukuba - ahsante sana!


Ofisi ya Mbunge 

Jimbo la Musoma Vijijini 

www.musomavijijini.or.tz 


P. O. Box 6

Musoma 


Tarehe:

Jumapili, 23 Feb 2025

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO 5 YA KILA MWANANDOA KUFAHAMU