WAKILI Eric Kidyalla ni moja ya makada waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania kugombea nafasi ya ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jimbo la Dodoma Mjini.
Alisema sababu iliyomsukuma kuchukua fomu hiyo ni kwa kuwa yeye ni kada wa Chama hicho hivyo aliona ni vyema kutumia haki yake ya kikatiba ili akifanikiwa aweze kutoa mchango wake katika kukitumikia Chama na wanaDodoma mjini akishirikiana na watendaji wengine.
Pia amepongeza Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia Jimbo la Dodoma mjini liweze kugawanyika jambo ambalo limetoa fursa kubwa kwa wanaCCM wengi kujitokeza kugombea.
"Jimbo la Dodoma mjini kijiografia lilikuwa kubwa hivyo kuridhiwa ligawanywe, Rais, Samia amefanya jambo jema na itatoa fursa kubwa kwa wananchi,"alisema Kidyalla
Kidyala akionesha fomu hiyo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments