UWT YACHANGIA SH.MILIONI 35 ZA KUSAIDIA DKT. MWINYI KUCHUKUA FOMU

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) akiwa na Makamu Mwenyekiti UWT Taifa Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC) pamoja na Katibu Mkuu wa (UWT) Ndg. Suzan Peter Kunambi (MNEC) wameendesha Harambee ya kuchangisha Fedha kwa ajili ya kumkabidhi Dkt. Hussein Ali Mwinyi aende kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar hapo kesho Tarehe 30 Agosti, 2025, katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Visiwani humo na kufanikiwa kuchangisha Shilingi Milioni Thelathini na Tano. ( Mil.35)


Hafla hiyo iliyofanyika Visiwani Zanzibar leo Tarehe 29 Agosti, 2025, ilihudhuliwa na Mgeni Rasmi ambaye ni Mke wa Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT, na Wanachama wa UWT/CCM.


Hapo kesho Agosti 30, 2025, UWT ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) pamoja na viongozi wa UWT na wanachama wa UWT/CCM watamsindikiza Dkt. Hussein Ali Mwinyi hadi katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Visiwani Zanzibar kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar.











Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WALIOKUWA WABUNGE WALIOPITIWA NA MKASI WA WAJUMBE

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

SPIKA MSTAAFU NDUGAI AFARIKI DUNIA

WAGOMBEA WALIOENGULIWA CCM LICHA YA KUONGOZA KURA ZA MAONI

RAIS SAMIA AMUONDOLEA POLEPOLE HADHI YA UBALOZI