Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Dk Samwel Shelukindo imeeleza kwamba, imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu, Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka ikitaarifu kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametengua uteuzi wa Humphrey Polepole, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kumuondolea hadhi ya ubalozi.
Aidha, Rais Samia kwa mamlaka aliyonayo chini ya sheria ya utumishi wa umma amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.
Comments