DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

Mwanaume nisikilize!

Umasikini unauma zaidi ukiwa mwanaume. Familia inakutazama tofauti sana hata kama haikuambii ila we fahamu tu kuwa kuna vile wanawaza na kukutazama. Ukiwa huna pesa kuna namna fulani watu wanakunyima heshima au wanakukadiria heshima. 

Ukiwa huna pesa hakuna anayejali unachosema haijalishi unasema point au jambo la maana kiasi gani. Na ukiendelea kutoa msisitizo ili point yako isikilizwe utaambiwa unapiga kelele au unaleta vurugu kwenye kikao.

Tunaishi katika Dunia ambayo haina huruma kwa mwanaume asiye na pesa. Dunia ni sehemu katili kwa mwanaume masikini si Kanisani si hospitalini kama huna pesa wewe si lolote si chochote hata aina ya maombi utakayopewa na heshima utakayopewa ni tofauti sana.

Hata Kanisani wewe hata uwe na wanawake 6 na vimada 6 lakini una hela heshima yako italindwa, lakini kama huna pesa utatengwa. Hata Kanisa haliwapi kipaumbele wala heshima watu wasio na pesa.

Mwanaume amka  kila siku ufanye kazi kwa bidii na kwa akili na maarifa — dunia ni katili sana kwa mwanaume maskini. 

Hii inaweza kuwa inaumiza kuisikia lakini ndio ukweli mchungu.

#boychildadvocate #relationship #couple #talaka #marriage #wanawake #mahusiano #NDOA #wanaume 

Remmy Cameroon 
Sauti ya wasio na sauti



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...