1. Tafuta mwanamke ambaye hata ukimtumia 5k atakwambia asante na sio kukusonya.
2. Tafuta mwanamke ambaye anajua kuna kupata na kukosa katika maisha.
3. Tafuta mwanamke ambaye anaweza kupunguza matumizi yake yasio ya lazima, ili aweze kuishi ndani ya kipato chako.
4. Tafuta mwanamke ambaye anaelewa kuwa sio yeye pekee anayehitaji usaidizi wako, wapo wazazi wako na ndugu wengine pia.
5. Tafuta mwanamke ambaye hawapi nafasi wanaume wengine.
6. Tafuta mwanamke ambaye ndugu zako watakuwa huru kuja kwako.
7. Tafuta mwanamke hakukatii tamaa hata unapopitia magumu.
8. Tafuta mwanamke ambaye anakutia moyo kila mara.
9. Tafuta mwanamke ambaye anatamani wewe ndio uwe baba wa watoto wake.
10. Tafuta mwanamke ambaye anaamini katika akili yako na maono yako.
11. Tafuta mwanamke ambaye anakupa amani katika maisha yako.
12. Tafuta mwanamke ambaye wewe ndio utakuwa kipaombele katika kila kitu.
13. Tafuta mwanamke ambaye atakufichia madhaifu yako.
14. Tafuta mwanamke ambaye atatangaza mazuri yako kwa rafiki na ndugu zake na sio mabaya yako.
15. Tafuta mwanamke ambaye mnapokuwa kwenye migogoro atakubali kutafuta suruhisho kwa amani.
16. Tafuta mwanamke atakukumbusha kuwasaidia ndugu zako.
17. Tafuta mwanamke ambaye hakuna anachokuficha katika maisha.
18. Tafuta mwanamke ambaye furaha yake ni kuona unafuraha.
19. Tafuta mwanamke ambaye unaamini hata siku ukiondoka duniani bado wanao watakuwa na mtu imara wa kuwaongoza.
20. Tafuta mwanamke ambaye kwenye shida anamkimbilia Mungu na sio waganga wa kienyeji.
21. Tafuta mwanamke ambaye nafasi yako kwake hatapewa mwanaume mwingine.
22. Tafuta mwanamke ambaye hata ukimpa pesa nyingi hazitumii hovyo.
23. Tafuta mwanamke ambaye atakushauri kuanziasha biashara na uwekezaji mwingine ili muwe na kesho nzuri.
24. Tafuta mwanamke ambaye anakusaidi katika kufanikiwa kwako.
25. Tafuta mwanamke ambaye ni mfariji katika maisha yako.
26. Tafuta mwanamke ambaye heshima yake kwako ni pale unapokuwa mbele yake na hata usipokuwa nae..
Comments