Kuna hali inazidi kushika kasi miongoni mwa wanaume wa kizazi hiki. Unakuta kijana anaonekana yupo sawa, ana tabasamu, ana marafiki, ana gari au hata ndoa lakini ndani yake kuna kilio kisichosikika, kuna mzigo Mkubwa usiobebeka, kuna uchovu wa kuishi maisha yasiyo yake.
Mwanaume wa sasa amekuwa kama mchezaji wa maigizo. Anaigiza mafanikio, anaigiza furaha, anaigiza mapenzi yote ili aonekane yupo juu, awe na heshima mbele ya marafiki, aonekane “mwanaume wa maana” mbele ya jamii. Lakini ni wangapi wameangamia kwa sababu hiyo?
Mashinikizo ya watu yamemweka mwanaume kwenye kona mbaya sana. Mwanaume anahisi hawezi kulalamika, hawezi kuomba msaada, hawezi kuanguka. Akilia anaitwa muoga. Akishindwa anaitwa dhaifu. Matokeo yake, anapigana na maisha peke yake mpaka anapotea kimya kimya. Depresheni inamla ndani kwa ndani, na hakuna anayejua.
Leo hii kijana anaoa si kwa sababu ya upendo, bali kutimiza matarajio ya watu,jamii,washikaji,na marafiki. Anatafuta mwanamke “mkali pisi kali wenyewe wanazita watoto wa mjini ” wa sura, sauti na shepu kubwa si kwa sababu anamfaa, bali kwa sababu anataka kuipa jamii picha ya kwamba ameweza. Anaingia gharama kubwa, anakopa ili afanikishe ndoa ya picha. Baada ya miezi sita au mwaka mmoja, mwanamke anamwacha. Mwanaume anabaki na deni, aibu na maumivu. Hapo ndipo depression inaanzia. Ndoto zinavunjika, moyo unachoka, akili inakataa kuendelea.
Lakini tunajifunza nini kwa hili?
Zamani mwanaume aliheshimiwa kwa busara, tabia na moyo wa kujenga familia. Hakuhitaji kuigiza. Hakuhitaji kumpata mwanamke mrembo ili athibitike. Alitafuta mwenza si kiungo cha kuonesha kwa jamii. Walipendana kwa dhati, wakavumiliana, wakajenga maisha kutoka sifuri bila mashindano. Na ndoa zao ziliishi miaka 30, 40, wengine mpaka 1000 kama babu na bibi yangu walivyo mpaka sasa wengine hadi kufa kwao.
Lakini mwanaume wa sasa ameondolewa kwenye mstari wa asili. Ameambiwa mafanikio ni gari, sura ya mke wake, likes kwenye Instagram, na video za harusi za kifahari. Ameambiwa kupenda si sifa bali udhaifu. Na sasa, tunaona matokeo yake: wanaume wanaanguka kisaikolojia, wanakata tamaa, wengine wanajiua,wengine wanawadunda wanawake mpka kuwaua
Na wewe mwanaume, hebu nisikilize hapa .......
👉 Si lazima uonekane tajiri ili uheshimiwe.
👉 Si lazima uwe na mpenzi “anayewakuna washikaji wako ” ili uthibitike.
👉 Si lazima uigize maisha usiyo na uwezo nayo.
Anza kuishi maisha ya kweli. Tafuta mwanamke wife material . Si lazima awe “perfect” kwa macho ya watu, bali awe “peace” kwa moyo wako. Si lazima aonekane mitandaoni, bali aheshimike ndani ya moyo wako. Si lazima awe wa kujionesha, bali awe wa kushikamana nawe hata dunia ikikataa.
Huna deni la kumfurahisha kila mtu. Huna deni la kuonekana. Unalo deni la kuishi maisha yako ya kweli
Credit to Annalisah Kihali
Comments